Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makonda Katibu mpya NEC Itikadi na Uenezi

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM akirithi mikoba ya Sophia Mjema.

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi akimrithi Sophia Mjema aliyeteuliwa kuwa mshauri wa Rais Samia Suluhu Hassan wa masuala ya wanawake na makundi maalumu.

Kuteuliwa kwa Makonda kunahitimisha taarifa zilizokuwa zikizagaa kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mrefu kuwa mwanasiasa huyo anaandaliwa kupewa nafasi ya Mjema.

Uteuzi wa Makonda kwenye nafasi hiyo unaakisi ule msemo wa dunia duara kwa kuwa wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alikuwa bosi wa Daniel Chongolo (aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni) na sasa Chongolo ndiye bosi wake.

Makonda alipokuwa Mkuu wa Mkoa katika moja ya mikutano alimtolea maneno ya ukali hadharani na kumzuia Chongolo asiseme chochote wakati yeye (Makonda) akizungumza

Katika mkutano huo, Chongolo alitii agizo hilo ingawa baadhi ya watu walionyesha kusikitishwa kwa alivyofanyiwa. Sasa ndani ya CCM ni Katibu Mkuu wa CCM na bosi wa Makonda.

Taarifa ya uteuzi wa Makonda, imetolewa leo Oktoba 22, 2023 na CCM muda mchache baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho.

Kulingana na taarifa hiyo, pamoja na Makonda, mwingine aliyeteuliwa na NEC ni Rabia Abdallah Hamid kuwa Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Rabia anamrithi, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Huyu ndiye Makonda

Jina la Makonda lilitambulika zaidi akiwa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alipowataja baadhi ya vigogo wa chama hicho aliodaiwa wanakiyumbisha kwa kuanzisha makundi ya kusaka urais Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Jina lake liliendelea kutawala katika uga wa kisiasa kwani mwaka 2014, aliteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba lililokuwa chini ya Uenyekiti wa marehemu Samuel Sitta aliyekuwa akisaidiwa (Makamu) na Rais Samia Suluhu Hassan.

Baadaye alliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na baadaye hayati John Magufuli alimteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, nafasi iliyompatia umaarufu.

Makonda aliachia nafasi hiyo mwaka 2020 baada ya kuamua kuwania ubunge wa Kigamboni akikabiliana na Dk Fautine Ndugulile aliyefanikiwa kutetea kiti chake.

Tangu mwaka 2020 alipoondoka madarakani Makonda aliamua kubadilisha aina ya siasa zake na kuwa kimya tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Januari mwaka 2020, Marekani ilitangaza marufuku ya mwanasiasa huyo na familia yake kutoingia nchini humo, ikimtuhumu kuvunja haki za binadamu.