Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makonda ambana meneja Ruwasa Monduli

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda akiwa ziarani Monduli. Picha na Mpiga Picha Wetu

Muktasari:

  • Tukio hilo lililitokea jana Jumatatu Mei 27,2024 wakati mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani humo, mwananchi mmoja alimuomba mkuu wa mkoa huo kumsaidia kuingilia kati upatikanaji wa maji safi.

Arusha. Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (Ruwasa), wilayani Monduli, Neville Msaki  amejikuta kwenye wakati mgumu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,  Paul Makonda baada ya kujikuta akishindwa kujibu maswali  kwa ufasaha na  hatimaye kuomba radhi.

Tukio hilo lililitokea jana Jumatatu Mei 27,2024 wakati mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani humo, mwananchi mmoja alimuomba mkuu wa mkoa huo kumsaidia kuingilia kati upatikanaji wa maji safi.

Makonda ambana meneja Ruwasa Monduli

“Mheshimiwa mkuu wa mkoa (Makonda), kuna kijiji kinaitwa Lendikija kuna mradi wa maji wa Sh 800 milioni, ambao hautoi maji, maji yanafunguliwa Monduli na kuishia kwenye makorongo kisha wananchi tunaletewa ankara, tumepeleka malalamiko hadi wizarani tunateseka,” amesema mwananchi huyo.

Baada ya maelezo hayo Makonda alimuita Msaki na kumuuliza  kama maelezo aliyoyatoa mwananchi huyo yana ukweli.

Akijibu swali hilo amesema, “Sasa hivi maji yanatoka mheshimiwa,” amesema Msaki.

Mahojiano yalivyokuwa

Makonda: Je, kuhusu ankara?

Msaki:      Ankara wanatakiwa kulipa kadri wanavyotumia maji.

Mwananchi: Mheshimiwa mkuu wa mkoa, mhandisi anajua suala lote na tumeangaika naye sana. Changamoto ya mradi ni bomba, kwa sababu maji yakifunguliwa mabomba yanapasuka na maji yanaishia kwenye makorongo.

Makonda: Mhandisi unaniambia maji yanatoka, mtumiaji anasema hayatoki na wewe unajua, kwa nini unanidanganya nani mkweli kati yako na mwananchi?

Msaki: Mimi ni mkweli mheshimiwa, kulikuwa kuna changamoto ya mabomba.

Kisha Makonda akamuuliza kwa mara nyingine mwananchi je maji yanatoka hayatoki? Akajibiwa kuwa hayatoki

Mwananchi: mheshimiwa yupo tayari kuongozana, maana kwa mwaka hatuna maji.

Makonda: Mhandisi mara yako ya mwisho kutembelea mradi ni lini?

Msaki: Januari mwaka huu

Makonda: leo mwezi wa ngapi?

Msaki : Wa tano.

Makonda: Una miezi mitano hujatembelea mradi, ndugu yangu ukinidanganya mimi utakuwa umefanya jambo ambalo hutokuja kulisahau katika maisha yako. Mimi waongo, wala rushwa na wazembe sina mswalie Mtume niambie tu ukweli.

“Hapa nilipo akili zangu naweza nikageuza safari tukaenda katika huo mradi, yaani naweza nikaacha kila kitu tukaenda, niambie kwa upendo maji yanatoka au hayatoki. Kama huna taarifa niambie tu sina taarifa sahihi nitakuelewa,”

Msaki: Mheshimiwa mkuu wa mkoa, sasa hivi sina taarifa sahihi.