Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makandarasi waeleza sababu kazi kuwa chini ya viwango

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa kamati ya mpito wa Umoja wa Chama cha Wakandarasi Tanzania (Tucasa), Samwel Marwa amesema miongoni mwa vitu ambavyo vitakavyopewa kipaumbele na umoja huo, ni kuhakikisha inaondoa dosari ya kazi kufanyika chini ya kiwango.

Dar es Salaam. Kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya miradi ya ujenzi kutekelezwa chini ya viwango, baadhi ya makandarasi wamesema wakati mwingine wanalazimika kufanya hivyo kutokana na maelekezo ya kazi husika.

Hata hivyo, suala hilo litakuwa kipaumbele cha Umoja wa Chama cha Wakandarasi Tanzania (Tucasa) kwa kuwashughulikia wakandarasi wote watakaobainika kufanya kazi chini ya viwango.

Akizungumza juzi Machi 24 katika mkutano maaluma wa chama hicho, Mwenyekiti wa kamati ya mpito wa chama hicho, Samwel Marwa amesema miongoni mwa vitu ambavyo vitapewa kipaumbele na umoja huo ambao ndio mwamvuli rasmi unaoshughulikia masuala ya makandarasi ni kuhakikisha inaondoa dosari hiyo.

Amesema kupitia kamati ya maadili ya chama hicho watakaobainika kufanya kazi chini ya viwango wataitwa na kuhojiwa sababu za kufanya hivyo na itakapothibitika kuwa amefanya hivyo kwa utashi wake atawajibishwa.

“Hatutafurahia kuendelea kusikia haya malalamiko lakini wengi wanasikiliza upande mmoja wa yule anayelalamika kwamba kazi imefanyika chini ya viwango, lakini ukifuatilia wakandarasi tunakutana maelekezo yanayosababisha mambo yawe hivyo.

“Ukiambiwa nunua glasi ya Sh2, 000 utafuata maelekezo, sasa shida inakuja pale unapopewa kiasi hicho cha fedha halafu ukatakiwa ununue glasi ya Sh10,000 sijui inawezekanaje. Kwa hiyo tukipata kesi za aina hii tutawaita wahusika watuelezee,” amesema Marwa.

Marwa alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuangalia upya uwezekano wa kuwa na kanuni zitakazotatoa mwongozo kwa  wakandarasi kulipwa kwa wakati ili waweze kutekeleza Kwa ufanisi miradi waliopewa kwasababu baadhi yao hushindwa  kufikia matarajio kutokana na kucheleshewa malipo.


Vivian Erick ambaye ni mjumbe wa umoja huo alisema kuanzishwa kwa chama hicho kutasaidia sana kupaza sauti ya pamoja kwenye mambo muhimu yanayohusu makandarasi.

 Amesema kupitia umoja huo wataendelea kusukuma ajenda ya wakandarasi wanawake kupata asilimia 30 ya zabuni zinazotolewa na Serikali jambo ambalo kwa sasa limekuwa likizungumzwa tu ila utekelezaji wake ni wa kusuasua.

“Mara kadhaa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akizungumzia suala hili lakini utekelezaji wake bado ni mdogo hivyo nikiwa kama mwanachama na mjumbe wa kamati ya mpito natamani jambo hili likafanyiwe kazi kikamilifu, wanawake tupate hizo asilimia 30 ya kazi zinazotolewa na Serikali,” amesema.