Majaliwa amkaribisha rasmi Biteko ofisini

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu wake na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko alipomkaribisha Ofisi Ndogo za Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Septemba 2, 2023.
Muktasari:
- Siku moja baada ya kuapishwa kwa Dk Doto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu amekaribishwa rasmi katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu zilizopo Magogoni jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemkaribisha Naibu wake, Dk Doto Biteko katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu zilizopo Magogoni jijini Dar es Salaam, huku akiahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.
Majaliwa amemkaribisha Dk Biteko leo Septemba 2, 2023.
Akizungumza baada ya kumkaribisha, Majalisa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiongezea nguvu Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kumteua Mheshimiwa Dk Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu ili waweze kusimamia uratibu shughuli za Serikali kwa pamoja.
“Naibu Waziri Mkuu tunakukaribisha sana hapa katika ofisi yetu na tunakupongeza kwa kuaminiwa na kupewa jukumu kubwa la Naibu Waziri Mkuu kwa lengo la kusimamia shughuli za Serikali. Nakuhakikishia kwamba una timu imara ambayo inatoa ushirikiano wakato wote,"
Dk Biteko aliapishwa Septemba Mosi mwaka huu katika Ikulu ndogo ya Zanzibar kushika cheo hicho ikiwa ni baada ya kuteuliwa siku tatu nyuma.
Mbali na kuwa Naibu Waziri Mkuu pia Dk Biteko amehamishiwa kuingozo wizara ya Nishati akiwa amehamishwa kutoka Wizara ya Madini alikokuwa akihudumi.
Akizungumza baada ya kukaribibwa ofisini, Dk Biteko ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano huku akiwaomba watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wafanye kazi kwa bidii ili maono ya Rais Samia na Watanzania yaweze kufikiwa.
Viongozi wengine walioshiriki mapokezi hayo ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako.
Wengine ni Naibu Waziri Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dk Jim Yonazi, Katibu Mkuu ofisi ya Waziri wa Nchi Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Syprian Luhemeja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu