Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama yatupa maombi ya kina Mdee

Muktasari:

  • Mahakama Kuu Dar es Salaam imetupa maombi ya Halima Mdee  na wenzake 19 kutokana na kasoro katika jina la mjibu maombi wa kwanza.



Dar es Salaam. Mahakama Kuu Dar es Salaam imetupa maombi ya Halima Mdee  na wenzake kutokana na kasoro katika jina la mjibu maombi wa kwanza.

Halima ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) na wenzake waliomba kibali cha kupinga kufukuzwa uanachama wa Chadema  katika mahakama hiyo.

Wajibu maombi walikuwa Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Chadema kupitia jopo la mawakili wake linaloongozwa na Peter Kibatala waliweka pingamizi wakiiomba Mahakama hiyo isiyasikilize maombi hayo, wakidai kuwa yana kasoro za kisheria huku wakibainisha hoja sita.