Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama yasimamisha usikilizaji kesi ya mjane wa Bilionea Msuya

Mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita

Muktasari:

  • Kesi ya mjane wa Bilionea Msuya imekwama kuendelea baada ya mmoja wa wazee wa baraza kuugua na Mahakama ikalazimika kusimamisha kwa siku mbili kumsubiri apone.

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeshindwa kuendelea na usikilizaji wa kesi ya mauaji ya mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara wa madini mkoani Arusha, Erasto Msuya, maarufu kama Bilionea Msuya; Miriam Steven Mrita na mwenzake, kutokana na kukosekana mzee wa baraza.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 103 ya mwaka 2018, Miriam na mwenzake RebiMiriam na Muyella wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji, wakidaiwa kumuua, Aneth Elisaria Msuya, ambaye alikuwa wifi yake (Miriam).

Aneth ambaye aliuawa Mei 26, 2016 kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kibada, Kigamboni, wilayani Temeke (wakati huo), jijini Dar es Salaam, alikuwa mdogo wa Bilionea Msuya,  aliyeuawa kwa kupigwa risasi eneo la Mijohoroni, Wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, Agosti 7, 2013 na

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Edwin Kakolaki ni Miriam na ipo katika hatua ya utetezi.

Leo Jumatatu, Novemba 6, 2023 kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea katika hatua ya maswali ya dodoso kwa shahidi wa nne wa upande wa utetezi.

Hata hivyo, imekwama na Mahakama kutokana na mmoja wa wazee wa baraza katika kesi hiyo kutokuwepo kwa sababu za kiafya na hivyo mahakama imelazimika kusimamisha usikilizwaji wale kwa siku mbili kumsubiri mzee huyo wa baraza apone.

"Kama manvyofahamu wote shauri hili limekuwa likiendeshwa kwa usaidi wa wazee wa baraza wawili, kwa bahati mbaya leo mmoja amepata shida ya kiafya  na wazee wanatengeneza corum (akidi)", amesema Jaji Kakolaki na kutoa amri ya ahirisho:

"Kwa sababu ana mapumziko ya siku mbili tunalazimika, kuahirisha shauri hili hadi tarehe 8/11/2023 tutakapoendelea. Shahidi unaonywa kuwa uko chini ya kiapo na unaotakiwa kufika mahakamani tarehe hiyo kuendelea na ushahidi wako."

Wazee wa baraza ni sehemu ya akidi katika kesi za jinai zinazosikilizwa na Mahakama Kuu kama Mahakama itaona ni muhimu kwa masilahi ya haki: kwa mujibu wa kifungu cha 265 Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, marekebisho ya mwaka 2022.

Kwa mujibu wa kifungu hicho wazee hao wa baraza wanapaswa kuwa wawili au zaidi kwa kadri Mahakama itakavyoona inafaa, na jukumu lao ni kumshauri jaji kwa masuala ya kiushahidi yasiyohusiana na utaalamu wa kisheria. Hata hivyo ushauri wao haumfungi Jaji katika uamuzi wake.

Upande wa mashtaka leo ilitarajiwa kumuuliza maswali ya dodoso shahidi huyo wa nne wa upande wa utetezi kuhusiana na ushahidi wake wa msingi alioutoa mahakamani hapo Ijumaa iliyopita.

Shahidi huyo wa nne wa upande wa utetezi ni Meneja Utawala na Matengenezo (ya magari ya wateja) wa kampuni ya uuzaji magari ya CMC Automobiles Limited, maarufu kama CMC Motors, makao makuu Dar es Salaam, Ernest Said Msuya.

Huyu ni shahidi wa mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Miriam, ambaye anafanya idadi ya mashahidi wa utetezi kuwa wanne akiwemo na mshtakiwa mwenyewe.

Katika ushahidi wake, akiongozwa na wakili wa mshtakiwa huyo, shahidi huyo aliieleza Mahakama kuwa gari aina ya Ford Rangers yenye namba za usajili T307 CBH, nayohusishwa katika kesi hiyo iko kwenye gereji yake tangu Mei 9, 2016.

Kwa mujibu wa ushahidi wa upande wa mashtaka, Miriam na mwenzake walikwenda Kigamboni kwa marehemu Aneth mara ya kwanza Mei 15, 206, wakiwa na gari aina ya Ford Rangers (T307 CBH) kwa ajili ya kufanya mipango ya mauaji hayo.

Ushahidi huo ulitolewa kwa nyakati tofauti na shahidi wa 22, Mkuu wa Upelelezi Mkoa (RCO) wa Arusha, Mrakibu Mwandaimizi wa Polisi (SSP) David Mhanaya kutokana na maelezo ya aliyekuwa mfanyakazi wa ndani wa marehemu Aneth, Getruda Peniel Mfuru.

Getruda ambaye ni shahidi wa  25 na wa mwisho wa upande wa mashtaka pia aalirudia maelezo hayo katika ushahidi wake, akidai kuwa washtakiwa walikwenda huko na akaonana nao mara tatu Kwa siku yofautitofauti yaani Mei 15, 18 na 23, 2016 wakiwa na magari tofauti likiwemo gari hilo.

Hata hivyo shahidi wa pili upande wa utetezi, Karim Mruma aliyejitambulisha kuwa ni dereva wa Miriam na familia yake aliieleza Mahakama kuwa yeye ndiye amekuwa akimuendesha Miriam na kwamba mwezi Mei wote Miriam hakutokea nje ya Arusha.

Pia alidai kuwa gari hiyo iliyotajwa washtakiwa kwenda nayo kwa Marehemu Aneth Mei 15, 2016, Iko katika gereji ya CMC tangu Mei 9, 2016 alipoipeleka kwa matengenezo na kwamba tangu tarehe hiyo mpaka sasa Iko katika gereji hiyo ya CMC Arusha.

Shahidi wa nne Msuya, naye ushahidi wake uliunga mkono maelezo hayo ya Mruma kuwa gari hiyo iko katika gereji yao tangu tarehe hiyo mpaka sasa.

Mbali na maelezo yake ya mdomo pia aliwasilisha vielelezo viwili kikiwemo kitambulisho chake cha kazi kuthibitisha kuwa ni mwajiriwa wa kampuni hiyo na wadhifa wake.

Pia, aliwasilisha mahakamani fomu ya usajili wa gari hilo kuonesha kuwa limekuwa likipelekwa katika gereji hiyo mara kwa mara kwa matengenezo, ikionesha tarehe mbalimbali za kupokelewa na kutoka na tarehe hiyo ya mwisho ya kupokelewa hapo mpaka sasa.

Alieleza kuwa kampuni hiyo ina matawi yake Arusha, Dodoma Mbeya Tanga na kwamba ofisi hizo zinafanya kazi kwa kuratibiwa na makao kwa kuwa kila kinachofanywa kwenye matawi hayo kinajulikana makao makuu kupitia mfumo wa mtandao wa kompyuta.

Shahidi huyo alielezea kuwa gari likipelekwa katika ofisi zao kwa matengenezo hupokewa na wataalamu kusajiliwa katika fomu maalumu ya kuonesha kumbukumbu za kupokelewa na kuorodheshwa katika  kadi maalum (job card) inayoelezea tatizo lake na tarehe iliyopokewa, dereva aliyelipeleka na namba zake za simu.

Alifafanua kuwa Jobcard ni nyaraka maalumu kwa ajili ya kuweka kumbukumbu za kupokelea gari la mteja na ni mali ya CMC, lakini mteja pia anapewa ya kwake na zote zinakuwa halisi.

"Kazi ya register ni kupokea gari na kurekodi muda na tarehe gari lilipoingia na umbali ambao limetembea (kilometa) wakati linaingia na zile inazokuwa nazo wakati linatoka, lengo likiwa ni kuwa na kumbukumbu za kuhakikisha usalama wa gari la mteja," amesema Msuya na kuongeza:

Kuhusu gari aina ya Ford Ranger T307 CBH, inaohusishwa katika kesi hiyo alisema kuwa hiyo gari anaifahamu, kwa kuwa waliiza kwa mteja na kampuni yao mwaka 2012, Arusha na kwamba toka waiuze wao ndio wanaifanyia matengezo mara kwa mara kila inapotokea hitilafu.

Baada ya kuwasilisha mahakamani fomu ya usajili wa gari hilo (regista) iliyopokewa kama kielelezo cha upande wa utetezi, shahidi huyo alianza kuisomea mahakama tarehe mbalimbali zinazoonesha jinsi gari hilo lilivyokuwa likiingia katika gereji hiyo Kwa matengenezo na kutoka mpaka tarehe hiyo ya mwisho.

"Gari hii liliingia CMC tarehe 9, mwezi wa 5 na ilitoka tarehe 10 Agosti, 2016, lakini likarudi tena tarehe hiyohiyo," amesema Msuya.

Alieleza kuwa wakati linatoka Agosti 10, 2016 Ikiwa na lilikuwa na kilomita 30, 569 (ulizokuwa imetembea) na kwamba wakati inarudi tarehe hiyo hiyo ulirudi ikiwa na kilomita 30573, zikiwa zimeongezeka kilomita nne na kwamba haijatoka tena mpaka leo.

Akifafanua kuhusu gari hiyo kutoka Agosti 10, 2016, takribani miezi mitatu baada ya mauaji ya Aneth, shahidi huyo alisema kuwa Polisi wa upelelezi Mkoa wa Arusha walikwenda kulichukua.

Alidai kuwa ingawa waliwaleza kuwa ni bovu haliwezi kutembea umbali mrefu lakini walilazimisha nao wakawaruhusu lakini muda mfupi baadaye wakalirudisha baada ya kuwashinda.