Mahakama yamuachia huru Mdude wa Chadema

Muktasari:
- Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imemuachia huru kada wa Chadema, Mdude Nyagali aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na dawa za kulevya baada ya mahakama kueleza kuwa ushahidi uliotolewa dhidi yake ni batili.
Mbeya. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imemuachia huru kada wa Chadema, Mdude Nyagali aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na dawa za kulevya baada ya mahakama kueleza kuwa ushahidi uliotolewa dhidi yake ni batili.
Leo Jumatatu Juni 28, 2021 ndio ilikuwa siku ya kusomwa hukumu ya Mdude ambaye akiwa mahakamani hapo amewaeleza baadhi ya wanachama wa Chadema kuwa kufungwa pingu imekuwa sehemu ya maisha yake.
"Haya ndio maisha yangu hizi pingu huwa hazipauki lakini kwa imani nitatoka tu! Ninawapongeza wafuasi wengine waliosafiri kutoka mikoa mbali kuja kuniunga mkono kwa kusikiliza hukumu yangu,” amesema Mdude kabla ya hukumu hiyo kuanza kusomwa.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi