Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Magonjwa yasiyoambukiza yaua watoto kwa asilimia 25 KCMC

Daktari bingwa wa watoto,  hospitali ya KCMC, Dk. Aisa Shayo akizungumza wakati wa uzinduzi wa semina ya siku 3 ya wataalam wa hospitali ya KCMC waliokutana kwa pamoja  ili kuweza kuelezea tafiti mbalimbali na matatizo ya magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Asilimia 25 ya vifo vya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini, KCMC vinatajwa kutokana na magonjwa yasiyoambukiza, huku sababu kubwa ikielezwa kuwa ni watoto kuzaliwa kabla ya umri wao (njiti).

Moshi. Asilimia 25 ya vifo vya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini, KCMC vinatajwa kutokana na magonjwa yasiyoambukiza, huku sababu kubwa ikielezwa kuwa ni watoto kuzaliwa kabla ya umri wao (njiti).

Magonjwa mengine yanayotajwa kushambulia watoto ni magonjwa ya moyo, saratani, kisukari na mapafu.

Hayo yamebainishwa leo Novemba 9 na daktari bingwa wa magonjwa ya watoto wa hospitali hiyo Dk Aisa Shayo wakati wa uzinduzi wa semina ya siku tatu hospitalini hapo.

"Ukiangalia vifo vya watoto wachanga asilimia 25-26 inasababishwa na watoto kuzaliwa njiti wakati kidunia inatakiwa tuwe kwenye asilimia chini ya 12, lakini bado tupo juu hivyo hatujaweza kufikia malengo ya milenia," amesema Dk Aisa.

"Vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto  chini ya mwezi mmoja hasa kwa watoto wachanga ndio yanayoongoza kwa vifo na ndio ina sabababisha kuwepo kwa ongezeko kubwa la vifo vya watoto kwa sababu asilimia yao ni kubwa," amesema.

Amesema vifo vingi vya watoto wachanga vinasababishwa na vitu vikubwa vitatu ambavyo ni mtoto kuzaliwa kabla ya muda wake, kuzaliwa na kushindwa kupumua (kushindwa kulia anapozaliwa) na tatu ni mtoto kupata maambukizi wakati anazaliwa.

Amesema ili kupunguza watoto wanaozaliwa na changamoto hizo ni vyema mama akiwa mjamzito aende  kliniki na vitu vyote muhimu vifanyike ikiwemo kuangaliwa magonjwa ya shinikizo la damu kama ana dalili za hatari ili kuzuia mtoto asizaliwe njiti.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Jairy Khanga amesema mkoa huo kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2023 wameweza kubaini idadi kubwa ya  watoto wenye magonjwa yasiyoambukiza wapatao 5,968.

"Tunategemea makongamano haya ya wataalam wa afya ili tuweze kupata mikakati mipya na afua mpya ambayo itawezesha kupunguza hali hii kwa kiasi kikubwa," amesema Dk Khanga.