Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madawati 8,800 yatolewa Geita, RC asema…

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Geita (RC), Martin Shigella ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa msaada wa kupitia mpango wa GGML wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) wa madawati yatakayokwenda kupunguza adha kwa wananfunzi.

Geita. Shule mbalimbali mkoani Geita zimepata msaada wa madawati 8,823 kutoka Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) ili kuchochea kiwango bora za elimu.

Mkuu wa Mkoa wa Geita (RC), Martin Shigella ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwa msaada huo kupitia mpango wa GGML wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) umekuja wakati muafaka.

Amesema kadiri shule nyingi zinavyoendelea kujengwa ndivyo hitaji la madawati linavyozidi kuonekana jambo ambalo GGML inajitahidi kutatua changamoto hiyo.

Shigella alipongeza kampuni hiyo kwa kuwa na mipango ya muda mrefu ya kuinua sekta ya elimu mkoani Geita na Tanzania nzima kwa ujumla.

"Ni furaha yangu kwamba tangu GGML ianze shughuli za uchimbaji hapa mkoani Geita, imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Serikali kutekeleza miradi kadhaa ya elimu, hasa ujenzi wa madarasa na shule," alisema

Mkuu huyo wa mkoa alikiri kuwepo kwa uhaba wa madawati katika shule mbalimbali hivyo kuwaomba wadau wengine mkoani humo kufuata nyayo za kampuni hiyo atika kuboresha mazingira ya kujisomea kwa wanafunzi.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong alisema ni muhimu kuboresha mazingira ya utoaji elimu nchini ili kufikia lengo namba nne la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.

"Kutoa elimu bora kwa wote ni msingi wa kujenga dunia yenye amani na ustawi. Elimu huwapa watu maarifa na ujuzi wanaohitaji ili kuwa na afya njema, kupata ajira. GGML inafurahi kuboresha maisha ya Watanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu," alisema.

Amesema malengo ya GGML katika kuboresha maisha ya Watanzania hususani kupitia uboreshaji wa sekta ya elimu, Strong alisema tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo mwaka wa 2000, GGML imeendelea kuwekeza katika nyanja mbalimbali zinazoboresha maisha ya jamii nzima ya Geita na Tanzania kwa ujumla.

Amesema GGML imewekeza kwa kuzingatia masuala muhimu kama vile afya, elimu, maji, barabara na miradi ya kuzalisha kipato cha kaya na kukuza uchumi wa Taifa.

"GGML imewekeza katika utekelezaji wa miradi endelevu ambayo inainufaisha jamii inayouzunguka mgodi. Kwa hiyo mchango huu wa madawati unadhihirisha jukumu la GGML kama mwananchi anayehitaji elimu bora kubadilisha maisha yake," alisema na kuongeza;

"Juhudi za GGML kujitolea kutekeleza miradi mbalimbali zinaendelea kuacha alama isiyofutika na kusaidia kuboresha maisha ya jamii kupitia uwepo wa kampuni hii mkoani Geita."