Mabasi ya abiria yagongana, yawaka moto abiria wakiwa ndani Same

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia kwa kuungua moto baada ya basi la abiria kuvaana uso kwa uso na basi dogo na kusababisha kuwaka moto wilayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro.
Ajali hiyo imetokea jioni ya leo Jumamosi Juni 28, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amethibitisha kutokea ajali hiyo.
"Kumetokea ajali, gari dogo la abiria na basi kubwa la abiria yamegongana kisha kuwaka moto, watu wameshindwa kutoka ndani ya hayo magari," amesema Mgeni.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.