Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabadiliko tabianchi kichocheo watu kuhama

Muktasari:

  • Changamoto za kimazingira kama vile ukame, mafuriko na kuongezeka kwa kina cha bahari vinavyosababisha binadamu na wanyama kuhamia maeneo mengine. Athari za mabadiliko ya tabianchi zinaongeza uhamaji, lakini mambo mengine kama migogoro na shughuli za kiuchumi pia zina mchango kwenye hilo.

Dar es Salaam. Changamoto za kimazingira kama ukame, mafuriko na kuongezeka kwa kina cha bahari na maji kuingia kwenye maeneo ya watu vinavyosababisha binadamu na wanyama kuhama kwenye maeneo yao.

Wadau wanasema si kila changamoto hizo hutokana na mabadiliko ya tabianchi, ila yanachochea kwa kiwango kikubwa kwenye kubadilisha mifumo ya maisha ya watu.

Mhadhiri kutoka Kituo cha Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabianchi cha  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Pius Yanda amesema maeneo yenye ukame,  mafuriko, pasipo na malisho ya wanyama watu wanahama kwenda kwenye fursa.

“Watu wanafuata shuguli nyingine za kiuchumi hasa vijana na wanaume, jambo linalowafanya wanawake kuathiriwa zaidi kwani wanahitaji kutunza kaya” amesema.

Akilizungumzia hilo, Mkurugenzi wa Kanda (Afrika na Mashariki ya kati), Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Dk Wessam El Beih amesema suala la uhamaji sio la mabadiliko ya tabianchi pekee, yanachochewa na shughuli za kiuchumi, migogoro na masuala ya kimazingira.

“Licha ya hayo tafiti za IDRC zinaonyesha watu wengi wanahama kutokana na masuala ya kiuchumi,  mabadiliko ya tabianchi yanachangia zaidi kuathiri shughuli hizo,” amesema.

Mwanahabari Baboki Kayawe akiwakilisha Chombo cha Habari cha Mesha cha nchini Kenya, amesema tafiti zinaonyesha wanawake na wasichana wameathiriwa zaidi.

“Wastani wa kaya moja kati ya nne kusini mwa Afrika inaongozwa na wanawake kwa sababu wanaume wamehama kwenda kutafuta maeneo yenye fursa, kutokana na waliyokuwa wakiishi awali kuathirika kwa namna moja ama nyingine,”amesema.

Amesema wanawake wanashindwa kuhama kutokana na majukumu kama walezi ya watoto, wanaangalia wagonjwa, utunzaji wa nyumba na kuedeleza familia.

“Wanawake wanategemea sana maliasili kwenye nchi za Afrika na hata mitaji yao ambapo kwa kiwango kikubwa vimeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi,” amesema Baboki na kutoa mifano ya utegemezi kwenye kilimo na nishati za kupikia.


COP28 na uhamaji wa watu

Katika mkutano mkubwa wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) uliomalizika hivi karibuni,  Dubai Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) miongoni mwa mda iliyojadiliwa katika pembeni mwa mkutano huo  ni athari za mabadiliko ya tabianchi na uhamaji wa watu.

Tafiti zinasema kuhama huku huchangiwa na kuongezeka kwa kina cha bahari na baadhi ya maeneo ya pwani kupotea, hali mbaya ya hewa kama mafuriko, ukame na upungufu wa maji, migogoro ya maeneo na ukuaji wa miji.

Takwimu za Internal Displacement Monitoring Centre (IDMC) zilionyesha hali mbaya ya hewa ilisababisha watu zaidi ya milioni 24 kuhama makazi yao, wakati takwimu za Benki ya Dunia (WB) zikitabiri kuongezeka kwa kina cha bahari kutafanya zaidi ya watu milioni 140 kukosa makazi.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) lilikadiria kuwa ifikapo mwaka 2050, athari za mabadiliko ya tabianchi kama mambo hayatabadilika sasa zitasababisha zaidi ya mamilioni ya watu kuhama.

Mtandao wa Growndswell ulibainisha kuwa zaidi ya watu milioni 216 watahama makazi yao, huku  watatu kati ya watano ni wa bara la Afrika, wawili kusini mwa jwangwa la Sahara na mmoja Afrika ya Kaskazini.

Takwimu hizi zinaonyesha Afrika itaathirika zaidi kama ambavyo mpaka sasa wadau wa nchi za Afrika ndio zinaathrika zaidi na athari hizi.


Nini kifanyike Wadau watoa mwelekeo                                                                     

Profesa Yanda amesema jambo kubwa ni  kuhakikisha mazingira ambayo wanahama watu yanawekewa miundombinu inayosaidia wao kubaki huko ili kuepusha migogoro maeneo wanayokwenda.

“Miradi kama ‘Jenga Kesho iliyo Bora’ (BBT), inasaidi kwa kiwango kikubwa ila inatakiwa kuenea maeneo mengi zaidi, miundombinu ya umwagiliaji na tafiti za kusaidia kilimo himilivu ni muhimu,”amesema.

Naye, Mwanzilishi wa mfuko wa  Doors of Hope, Shamim Nyanda amesema ili kuhakikisha ustahimilivu wa walio hatarini zaidi hasa wanawake, kunahitajika kuwezeshwa makundi hayo kupitia elimu na mafunzo ya ujuzi ili kukuza uwezo wao kwenye kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na majanga mengine ya asili.

Amesema, “Utekelezaji wa sera zinazozingatia jinsia pia ni muhimu katika kutambua changamoto wanazokutana nazo wanawake. Upatikanaji wa rasilimali na usaidizi wa kifedha unaweza kuimarisha uwezo wao wa kukabili hali hiyo,”amesema.

Amesema ushirikishwaji katika michakato ya kufanya maamuzi katika ngazi zote za uongozi husaidia kuongeza ufahamu kuhusu uhusiano wa jinsia na mabadliko ya tabianchi,  pia ni muhimu kukuza ushirikiano wa kimataifa na kusaidia wanawake katika kustahimili hali hiyo.

Baboki ameshauri kuandaliwa kwa mpango jumuishi unaozingatia jinsia jambo linalohitaji rasilimali na linapaswa kufanywa haraka. Pia alishauri taasisi za utafiti kufanya tafiti na kuja na masuluhisho kwa jamii juu ya kukabiliana na hali hiyo.

Amesema:“Watafiti na taasisi za elimu zisitoe tu tafiti kwa ajili ya vyeti, zinatakiwa kuhakikisha zinanufaisha jamii. Mabadiliko ya sera na uenezwaji wa sera mpya ufanywe na wadau na vyombo vya habari, wanahabari wakuze uhusiano kati ya jamii na watafiti.

Dk Wessam El Beih wa IDMC, amesema baadhi ya sera zinazoweza kuwalinda watu walio hatarini zaidi ya kuhama ni kuimarisha ustahimilivu na uwezo wa kukabiliana na hali hii kwenye jamii katika maeneo ya vijijini, kwa kurahisisha ufikiaji wa huduma za msingi, fursa za maisha na hatua za kupunguza athari kama mafuriko na ukame.

“Kuimarisha ulinzi wa kisheria na kijamii kwa wahamiaji na watu waliohamishwa. Kuwezesha njia salama, na taratibu za kuwapokea wahamiaji” amesema.

Dk Wessam amesema bila shaka kuna haja ya kuandaa mbinu endelevu za kushughulika na sababu za msingi za mabadiliko ya tabianchi, kwa kupunguza uzalishaji wa hewa chafu.

Ameshauri zaidi elimu ipatikane kwa watu kufahamu visababishi vya mabadiliko ya tabianchi, ili wakabiliane na hali hiyo na kuiepuka.


Habari hii imewezeshwa na MESHA na Ofisi ya Afrika ya IDRC Mashariki na Kusini.