Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lori latumbukia mtoni, mmoja amefariki dunia

New Content Item (22)
New Content Item (22)

Muktasari:

  • Daraja lililopo eneo la Mbecha Barabara ya Mbecha-Ndanda, Kata ya Nanganga wilayani Ruangwa limekatika na kusababisha lori kutumbukia mtoni na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Ruangwa. Mwanamke mmoja amefariki dunia baada ya gari alilopanda kutumbukia katika Mto Lukuledi uliopo eneo la Mbecha, mkoani Lindi.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatano, January 17, 2024, Mkuu wa Mkoa wa Lindi (RC), Zainabu Telack amesema lori hilo aina ya Howo likiendeshwa na Jafari Magumba, mkazi wa Kitangili, Shinyanga, lilitumbukia mtoni baada ya daraja kukatika.

Daraja hilo lipo katika eneo la Mbecha Barabara ya Mbecha -Ndanda kata ya Nanganga Wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Telack amemtaja marehemu ni Debora Lutubija (28), mfanyabiashara na mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam.

"Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani kwetu ndio zimesababisha kutokea kwa ajali hii kutokana na kukatika kwa daraja hili," amesema.

"Hii barabara ni ya changalawe kwa hiyo mvua ikinyesha udongo ukishaloana unasababisha kubaki na unyevunyevu ndio sababu ya kukatika kwa daraja hili," amesema mkuu huyo wa mkoa

Telack amesema mwili wa Deborah umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha kituo cha afya Luchelegwa.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema dereva alikuwa anakwepa daraja la Ruangwa -Nanganga ambalo limejaa maji, “sasa dereva akaona bora apitie barabara hii ya Mbecha-Ndanda, mimi niombe Serikali kujitahidi kulijenga hili daraja kwa haraka."