Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lazima uvaaji wa barakoa kwenye daladala

Muktasari:

  • Mkuu wa mkoa wa Dar es  Salaam, Amos Makalla amesema uvaaji wa barakoa kwa wanatumia usafiri wa umma ni lazima kuanzia sasa na siyo hiari tena.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema kuanzia sasa siyo hiari kuvaa barakoa bali ni lazima kwa watu wanaotumia usafiri wa umma au wanaokwenda au kuingia katika vituo vya mabasi.

Makalla ameeleza hayo leo, Jumatatu Agosti 2, 2021 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu mwenendo wa uchukuaji wa tahadhari kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema wamefanya tathimini na kubaini kuna baadhi ya maeneo ikiwemo vyombo vya usafiri kuna ulegevu wa uchukuaji wa tahadhari.

Makalla ametoa msimamo huo, akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam, akisisitiza kuwa ugonjwa wa corona upo na wagonjwa wapo katika hospitali za Serikali na binafsi ,  lazima wananchi waendelee kuchukua tahadhari za kujikinga.

"Ukiingia kwenye gari, kivuko lazima uvae barakoa, hili ni moja ya sharti. Nimefanya survey ukienda Kivukoni Feri mtu anaingia na barakoa kwa sababu ya usimamizi akiwa ndani anaivua, akitaka kutoka anaiva tena," amesema Makalla.

"Tumepokea taarifa ya utekelezaji wa mwongozo wa Wizara ya Afya kuhusu kujikinga na corona kutoka kila wilaya tumebaini kuna ulegevu wa utekelezaji wa jambo hili. Sasa utekelezaji wa hiari haupo tena bali ni lazima ili kukabaliana na changamoto hii," amesema Makalla.

Makalla amesema wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma, vivuko lazima kuzingatia jambo hilo, akisema suala la kuchukua tahadhari ikiwemo kuvaa barakoa siyo hatua ya kuiridhisha mamalaka husika bali usalama wa mwananchi.

"Wamilili watusaidie hili, wahakikishe wanawaeleza watu kuhusu kuchukua tahadhari kwenye vyombo vya usafiri. Wakati wowote tutakuwa tunasimamisha gari na kuanza ukaguzi na tukiona watu hawajavaa mmiliki ueleze," amesema Makalla.

Makalla amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kutowaruhusu au kuwabeba abiria wasiovaa barakoa kwa mujibu wa mwongozo wa Wizara ya Afya, akisisitiza jambo hilo ni lazima kwa hatua ya sasa na sio hiari.

Pia Makalla amekazia suala la abiria kukaa kwenye daladala kulingana na idadi ya viti vilivyomo' level seat' akisema jambo hilo ni muhimu na wamiliki vyombo hivvyo vya usafiri kuanzia mwendokasi hadi daladala kulizingatia.

Kuhusu wanafunzi Makalla amesema lazima wavae barakoa wakati wa kutumia usafiri wa umma, huku akisema wao wataruhusiwa kusimama watano katika daladala akitaka utekelezaji huo ufanyike kikamilifu.