Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kizimbani kwa wizi wa mtoto Moro

Lilian Stanley akisindikizwa na askari polisi baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro jana akituhumiwa kuiba mtoto mchanga Kanisa la Ufufuo na Uzima Kihonda.

Muktasari:

Lilian Stanley, mtuhumiwa wa kuiba mtoto mchanga mjini hapa amefikishwa mahakamani.

Morogoro. Lilian Stanley, mtuhumiwa wa kuiba mtoto mchanga mjini hapa amefikishwa mahakamani.

Lilian ambaye ni mkazi wa Uwanja wa Taifa mjini hapa, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kwa tuhuma ya kuiba mtoto mchanga mwenye umri wa mwezi mmoja.

Anatuhumiwa kumwiba mtoto huyo kutoka kwa mama yake, Neema Seleman (27) katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Kihonda mkoani hapa.

Mashtaka ya Lilian yalisomwa na mwendesha mashtaka wa Serikali, Evelyne Ndunguru mbele ya hakimu mkazi mfawidhi, Maua Hamduni. Mtuhumiwa anadaiwa kuwa Desemba 24 mwaka jana alimwiba mtoto huyo kutoka kwa mama yake wakiwa kanisani.

Evelyne alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na sheria na kanuni ya adhabu.

Akitaja shtaka hilo, hakimu Hamduni alisema dhamana ipo wazi kwa mtuhumiwa na kwamba kesi hiyo imetajwa kwa mara ya pili baada ya mshtakiwa kufikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Desemba 29.