Kivuko MV Nyerere sasa kipo ufukweni

Muktasari:
- Kazi ya kukivutia ufukweni kivuko cha Mv Nyerere inaendelea katika mwalo kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.
- Kivuko hicho kimesogezwa hadi umbali usiozidi hatua 30 kutoka nchi kavu
Ukara. Kivuko cha Mv Nyerere kimevutwa hadi umbali usiozidi hatua 30 kutoka nchi kavu ya ufukwe wa Ziwa Victoria katika kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.
Kazi ya kukivutia nchi kavu kivuko hicho kilichopinduka Septemba 20, 2018 inafanywa na wataalam wa uokoaji kutoka vikosi vya ulinzi na usalama wakishirikiana na wenzao kutoka makundi mbalimbali.
Wataalam hao wameanza kazi hiyo tangu saa 5:21 asubuhi leo Septemba 28 wakitumia mitambo maalum ya kuvuta vitu vizito.
Ili kisianguke, kivuko hicho kimeegemezwa kwenye meli kubwa ya mizigo ya Mv Nyakibalya inayosindikizana nayo sambamba kuelekea ufukweni.
Soma Zaidi: