Kinana aingilia kati migogoro ya madiwani Moshi
Muktasari:
Makamu mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amesema atazungumza na Waziri wa Tamisemi kufika mkoani Kilimanjaro kushughulikia mgogoro wa madiwani na Mkurugenzi wa Halmaahauri ya Moshi na Moshi Manispaa ambao umepelekea kung'olewa kwa Meya.
Moshi. Makamu mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amesema atazungumza na Waziri wa Tamisemi kufika mkoani Kilimanjaro kushughulikia mgogoro wa madiwani na Mkurugenzi wa Halmaahauri ya Moshi na Moshi Manispaa ambao umepelekea kung'olewa kwa Meya.
Kinana ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 26, 2022 wakati akizungumza kwenye mkutano wa kujitambulisha mkoani Kilimanjaro, ambapo amesema migogoro hiyo haileti picha nzuri kwa wananchi.
Hivi karibuni Madiwani wa Halmaahauri ya Moshi wakiongizwa na mwenyekiti wa Halmaahauri hiyo, Moris Makoi walitoa malalamiko wakidai mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kastory Msigala anakiuka taratabu na kifanya maamuzi bila kuwashirikisha madiwani wakati madiwani wa Manispaa ya Moshi wakimng'oa Meya Juma Raibu wakimtuhumu kwa makosa mbalimbali.
Amesema atazungumza na aziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa ili afike mkoani hapo kushighulikia migogoro hiyo na kuipatia ufumbuzi.
"Niliwaona madiwani wa Moshi Vijijini wakigombana nje ya ofisi, pale ni nje ya vikao si vizuri, vitu kama hivi vipelekwe kwenye vikao, nitamuomba waziri wa Tamisemi afike hapa asikilize matatizo ya Moshi ili hali iweze kutulia" amesema Kinana.
Kinana yupo katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Kilimanjaro, ambapo ameambatana na Katibu wa Halnashauri Kuu ya CCM Taifa, itikadi na uenezi Shaka Hamdu Shaka pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) CCM, Kanali mstaafu, Ngemela Lubinga.