Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinana afichua siri CCM kuendelea kubaki madarakani

Muktasari:

  • Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara, Abdulrahman Kinana ameanza ziara katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM yam waka 2020/25.

Katavi. Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara, Abdulrahman Kinana amesema siri ya chama hicho kuendelea kubaki madarakani kunatokana na aina ya demokrasia yake, uhuru, uwazi na utoaji maoni.

 Akizungumza na wakazi wa Mkoa wa Katavi, leo Jumatatu Julai 25, 2022, amesema ustawi huo unasababisha demokrasia ndani ya chama hicho kutoa fursa sawa kwa kila mwanachama kuwa huru kuchagua au kuchaguliwa.

"Siri ya Chama Cha Mapinduzi kuendelea kutawala nchini ni kutokana na demokrasia iliyojengeka ndani ya chama chetu, watu kuwa huru kuchagua na kuchaguliwa," amesema

Amewataka wana CCM mkoani Katavi kujitokeza na kushiriki kwenye uchaguzi unafanyika mwaka huu ikiwa sehemu ya kudumisha mfumo huo.

"Uongozi wetu si wa kisulutani wala kifalme, ukimaliza miaka yako mitano kiti kiko wazi, tunaingia kwenye uchaguzi hata mimi mwenyewe nafasi niliyopata nimechaguliwa," amesema

Chama hicho kiko kwenye uchaguzi wa ndani ngazi ya wilaya, mikoa na taifa ambapo shughuli za uchukuaji na urejeshaji fomu utahitimishwa Agosti 10, 2022.