Kinana awapa ‘tano’ CCM Katavi

Muktasari:
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)- Bara, Abdulrahman Kinana amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 katika kuwaletea maendeleo ya kijamii wananchi wa Katavi
Katavi. Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)- Bara, Abdulrahman Kinana amesema ameridhishwa na kasi ya viongozi wa Wilaya ya Katavi katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/25 kwa usahihi na uaminifu.
Pia, kimefurahishwa na ushirikiano uliopo kati ya watendaji wa Serikali Kuu na halmashauri za wilaya katika kuhamasisha wanachi kufanya kazi kujiletea maendeleo.
Ameyasema Jumatatu Julai 25, 2022 wakati akizungumza na wanachama wa CCM mjini Mpanda mkoani Katavi katika ziara yake aliyoianza katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya.
"Siri ya mafanikio haya ni kutokana na kuwepo mahusiano, mashirikiano na kuaminiana kwa watendaji wenye dhamana, naomba muendelee na mwendo huo kusukama maendeleo,” amesema.
Kinana amebaini hata matumizi ya fedha zinazoletwa toka Serikali Kuu zimekuwa zikisimamiwa kwa uadilifu jambo aloamini wananchi wataendele kujenga imani na sera ya chama hicho.