Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinachosababisha kiungulia

Kinachosababisha kiungulia

Muktasari:

  • Kiungulia ni dalili inayompata mtu kwa kuhisi hali ya kuwaka moto katika eneo la pembeni ya mfupa wa titi au katikati ya chembe ya moyo.



Kiungulia ni dalili inayompata mtu kwa kuhisi hali ya kuwaka moto katika eneo la pembeni ya mfupa wa titi au katikati ya chembe ya moyo.

Kiungulia ni kichochezi kikubwa cha maumivu makali kwa muathirika wa vidonda vya tumbo.

Kutiririshwa kupita kiasi kwa tindikali ya mfuko au tumbo la chakula ndiyo chanzo cha kuleta shambulizi na mkereketo unaosambaa kuanzia eneo la chini la bomba la chakula mpaka kooni.

Kiungulia ni moja ya dalili inayojitokeza kwa watu wengi bila kuchagua umri wala jinsia.

Tatizo hili likiendelea kuwapo zaidi ya mara mbili kwa moja huwa ni ugonjwa ujulikanao kitabibu kama Gastroesophageal reflux disease (GERD).

Takwimu za kituo cha udhibiti magonjwa cha Marekani kinaonyesha kuwa karibu watu milioni 15 nchini humo hupata tatizo hili kila siku.

Chanzo kikubwa cha kujitokeza kwa tatizo hili ni mienendo na mitindo ya kimaisha tunayoishi na kufanya kila siku. Ingawa yapo pia mambo mengine yasiyoepukika husababisha tatizo hilo.

Kwa kawaida chakula tunachokula hutafunwa mdomoni na kupita katika bomba la chakula na kufika katika mfuko wa chakula(stomach) ambapo huwamo na vitu mbalimbali vinavyokisagana ikiwamo tindikali ya hydrochloric.

Tindikali hii husaidia kuvunja vunja chakula, lakini pale inapotokea umekula mlo na kushiba inaweza kuzalishwa kwa wingi na kusababisha kurudi nyuma.

Inaporudi nyuma huelekea katika bomba la chakula kupitia kifungo cha bomba la chakula na mfuko wa chakula.

Katika bomba la chakula na tumbo huwapo misuli inayobana na kuwa kama mlango wakutokea, pale unapokula mlo mwingi na kushiba tindikali inayotiririshwa kwa wingi kusaga chakula hicho huleta uchokozi na kusababisha kukereketa katika kifungo hicho.

Hii ndio maana mtu hupata maumivu, kukereketwa na kuwaka moto chini ya kifua au katika chembe ya moyo.

Tatizo hilo huongezeka zaidi mara tu baada ya kumaliza kula, nyakati za usiku, mtu akiwa amejilaza huku wajawazito hulipaya kwa sababu (wakati wa ujauzito homoni za kike husababisha kifungo cha bomba la chakula kuwa legevu).

Vyakula ambavyo mara kwa mara vimekuwa vikichangia tatizo hili ni pamoja na kula mlo mwingi wenye viungo vingi, mafuta mengi, vyakula vyenye tindikali nyingi na mlo wenye kiasi kikubwa cha wanga na unywaji pombe.

Dalili za mtu mwenye kiungulia ni pamoja na kuhisi kuwaka moto katika chembe ya moyo, mara zingine huambatana na maumivu yanayoweza pia kusambaa katika shingo, koo na katika kingo za taya.

Maradhi kama ya moyo, bomba la chakula na tumbo la chakula yanaweza kusababisha kiungulia.

Tatizo hilo linaweza kudhibitiwa kwa kuepuka kula vyakula vyenye asili ya tindikali na matibabu ya dawa za tiba zinazokata makali ya tindikali pamoja na kudhibiti mfumo wa chakula kutoa tindikali.