Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kina Mbatia, Selasini wagongana msiba wa Mrema

Muktasari:

  • Mrema ambaye anatarajiwa kuzikwa Agosti 24 mkoani Kilimanjaro alifariki dunia Jumapili ya Agosti 21, 2022, saa 12.15 asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam huku akiacha mke na watoto watano ambapo watatu kati yao ni wanaume.

Dar es Salaam. Viongozi wa chama cha NCCR Mageuzi wanaohasimiana wamekutana katika msiba wa aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema, ambapo wamemwelezea marehemu kama kiongozi aliyetoa mchango kwenye chhama chao.

Mgogoro huo ulilipuka Mei 21 mwaka huu, baada ya viongozi wa NCCR Mageuzi kumsimamisha Mwenyekiti wao, James Mbatia na Makamu Mwenyekiti pamoja na Sekretarieti yake yote na kwamba atatakiwa kujieleza katika mkutano mkuu utakaofanyika Septemba.

Hata hivyo, upande wa Mbatia ulipinga huku nao ukitangaza kuwasimamisha viongozi, akiwemo Katibu Mkuu wa chama hicho, Martha Chiomba.

Leo Agosti 23 katika msiba wa Mrema Salasala jijini hapa, baadhi ya viongozi wa pande mbili wa chama hicho wamekutana na kuanza kumwagia sifa Mrema.

Mrema ambaye anatarajiwa kuzikwa Agosti 24 mkoani Kilimanjaro alifariki dunia Jumapili ya Agosti 21, 2022, saa 12.15 asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam huku akiacha mke na watoto watano ambapo watatu kati yao ni wanaume.

Akitoa sifa zake kwa Mrema, Joseph Selasini ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya chama hicho, amesema hadhani kama katika siasa za upinzani amewahi kuwapo mwanasiasa wa kuvuta hisia za watu wake kama ilivyokuwa kwa Mrema.

Selasini ambaye katika kuongea kwake alimtambua Mbatia kama mwanachama wao alisema kampeni za Mrema za Urais ziliibua majabari ya siasa na hadi sasa hayajawahi kufutwa huku akieleza kuwa kambi ya upinzani bungeni mwaka 1995 haijaweza kusahaulika.


"Mwaka 1996 kuna wabunge waliapa mara mbili baada ya wabunge wa NCCR Mageuzi kujenga hoja kuwa viapo walivyoapa ni batili na Andrew Chenge akiwa Mwanasheria mkuu wa Serikali akaridhika, wote walikuwa weapa wakaapa upya," amesema.

Amesema wakati Mrema akigombea urais alikuwa msaidizi wake huku kazi zote za kampeni wakishauriana nini kifanyike na kisifanyike na kipi kisemwe na kipi kisisemwe.

Amesema jambo lingine ambalo halitakuja kusahaulika wakati Mrema akiwa mwenyekiti wa NCCR Mageuzi ni namna wabunge wake walivyojenga hoja ikiwemo ile ya kupinga kubadilishwa kwa sura za viongozi katika noti (fedha).

"Mbunge wa NCCR mageuzi alijenga hoja, sheria ikarekebishwa, ndiyo hiyo ipo mpaka sasa," alisema Selasini.

Wakati yeye akimueleze hivyo, Mbatia aliyejitambulisha kama Mwenyekiti amesema Mrema katika maisha yake alikuwa na sifa ya uthubutu na kutenda analoamini na kusemea watu bila kuyumba.

Amesema mwaka 1985 hadi 1995 akiwa mbunge wa Moshi vijijini alisimama kuzungumzia zao la kahawa na kuzungumzia matatizo ya watu wa jimbo lake.

Pia alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kazi alizofanya zinaendelea kuishi mpaka leo ikiwemo vituo vya polisi kujenga fikra za ulinzi shirikishi zinaishi hadi leo

"Pia Alikuwa mtu wa kusuluhisha migogoro mingi ikiwemo ya kidini, alikuwa na sifa ya uthubutu alipoona wanagongana fikra na wenzake ndani ya baraza la mawaziri aliamua kutoka na hata alipohama CCM hakuwahi kuhama hadi umauti umemkuta.

 Kwa upande wake Anthony Komu amesema amefanya kazi na Mrema kwa karibu akiwa kama msaidizi wake na mwaka 1995 alipogombea urais yeye ndiye alikuwa Katibu.

"Tofauti na viongozi wengine niliowajua, Mrema alikuwa mtu wa kujishusha sana kwenda kwa watu ambao anawahudumia.

Majonzi yatawala

Majonzi na vilio vimetawala katika nyumba ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustine Lyatonga Mrema (77) baada ya mwili wake kuwasili ukitokea hospitalini.

Mwili wa Mrema umefikishwa nyumbani kwake saa 11 jioni huku ukipokelewa na familia, ndugu na majamaa waliofika kutoa pole kwa wafiwa.

Mwili huo unatarajiwa kulala hapo kabla ya shughuli ya ibada inayoyotarajiwa kufanyika kesho.

Kwa upande wa Dar es Salaam, Mrema ataagwa kesho katika kanisa Katoliki lililopo eneo la Salasala jijini hapa kabla ya kusafirishwa kwenda Mkoani Kilimanjaro.

Mrema katika uhai wake aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alizaliwa Desemba 31, 1944, Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Pia mwanasiasa huyo aliwahi kuwa mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.