Kilichomkimbiza Dayna kwa Sheddy ni Diamond Platnumz

Msanii Dayna Nyange
Muktasari:
- Wakati Dayna anatoka kwenye muziki, kazi zake nyingi zilipikwa na mtayarishaji Sheddy Clever ndani ya Studio za Burn Record ambaye alitengeneza wimbo uliomtoa kimataifa Diamond Platinumz, “Number One”.
Dar es Salaam. Nyota wa kike anayetamba na wimbo Chovya, Dayna Nyange anasema aliacha kufanya kazi kwa mtayarishaji Sheddy Clever baada ya kumpa biti yake Diamond Platnumz.
Wakati Dayna anatoka kwenye muziki, kazi zake nyingi zilipikwa na mtayarishaji Sheddy Clever ndani ya Studio za Burn Record ambaye alitengeneza wimbo uliomtoa kimataifa Diamond Platinumz, “Number One”.
Dyna anasema tatizo lilikuwa baada ya Clever kutumia ‘Beat’ yake kutengeneza wimbo wa Number One bila kumshirikisha.
“Sheddy nimefanya naye kazi kwa muda fulani lakini baada ya kutokea tofauti nikaamua kutafuta mtayarishaji mwingine ambaye ni mtu sahihi, nafanya kazi na T -Touch, anafanya kazi nzuri na anajua nini anataka, sijafikiria kutoka kwenda sehemu nyingine na siwezi kufanya kazi tena na Sheddy,” anasema.