Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikwete aonya ARV za mitaani

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Hai. Rais mstaafu Jakaya Kikwete amewatahadharisha Watanzania akiwataka kuchukua dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV) katika hospitali rasmi zinazotambuliwa na Serikali.

Amesema Serikali inaendelea kuhakikisha zinapatikana mashine nyingi za kupima kiwango cha virusi na ARV, ambazo hutolewa bure.

Kikwete alisema hayo jana, alipowaaga wapanda mlima 35 na waendesha baiskeli 26 walioanza safari ya kuupanda Mlima Kilimanjaro kwa siku saba kupitia geti la Machame.

Upandaji huo mlima unalenga kuchangisha fedha kwa ajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi kupitia kampeni ya 'GGM Kili change 2023'.

“Serikali inahakikisha dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi zinapatikana bure haziuzwi, ukisikia mahali zinauzwa anakutapeli na kwa sababu zinapatikana hospitali bure, ukienda kununua mtaani huko unauziwa hata zile wanazoweka unga wa muhogo,” alisema.

Aliwapongeza wapanda mlima akisema ushiriki wao unadhihirisha wana dhamira ya dhati ya kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.

“Tulitoka mbali, wakati wa Mzee Mkapa (Benjamin) alianza nayo ikiwa asilimia nane, alipoondoka akaniacha ikiwa kwenye asilimia saba, tumepambana mpaka kufika 2015 tukiwa kwenye asilimia 5.1 na lengo lililowekwa katika malengo ya milenia ni kwamba tufikishe mapambo na asilimia 5.4. na sisi tukafikia asilimia 5.1,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Dare, Dk Lilian Mwakyosi alishauri ili kudhibiti watu kuchukua dawa maeneo yasiyo rasmi Serikali ifanye iwe rahisi watu kupata huduma popote mpaka maduka ya dawa kwa kuwa siyo kila mtu anapenda kwenda vituo vya afya.

Alisema kuna dhana potofu mitaani kuwa kuna watu wanaweza kutibu VVU wakati suala hilo siyo kweli. Alisema utoaji wa dawa kiholela hauruhusiwi kwa kuwa ni mpaka kuwa na kibali maalumu cha kuanzisha huduma ya kutoa ARV kwenye kituo, hivyo kuna uwezekano wapo wanaouza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa GGML, Terry Strong aliishukuru Serikali kwa kuwaunga mkono katika kampeni ya kupambana na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Ummy Nderiananga, alisema mwaka wa fedha uliopita Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) ilitengewa Sh14 bilioni, sasa imetengewa Sh25 bilioni.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, alisema kutokana na jitihada zinazofanywa na Serikali mkoani humo, maambukizi ya VVU yamepungua kutoka asilimia saba mwaka 2003 hadi kufikia asilimia 2.6 mwaka huu.

"Mafanikio yaliyopo ni matokeo ya juhudi za pamoja za sekta za umma na binafsi. Tutafikia malengo yetu kufika mwaka 2030 kutokuwa na maambukizi kabisa," alisema.