Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ‘waliotumwa na afande’ yaanza kuunguruma Dodoma

Watuhumiwa wa kubaka na kulawiti wakiwa katika mstari katika kordo za Mahakama ya Kanda Dodoma. Picha na Hamis Mniha

Muktasari:

  • Watuhumiwa wanne, wakiwamo askari wa JWTZ na Jeshi la Magereza, wanaokabiliwa na mashtaka ya ubakaji wa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbile binti wa Yombo Dovya, kesi yao imeanza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.



Dodoma. Watuhumiwa wanne wakiwamo askari wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Magereza wanaotuhumiwa kwa ubakaji kwa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbile binti wa Yombo Dovya jijini Da es Salaam, wameingia chumba cha Mahakama.

Kesi hiyo iliyokuwa imepangwa kuanza saa 8:00 mchana wa leo Jumanne, Agosti 20, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, wameingia kwenye chumba cha Mahakama saa 10:20 jioni.

Watuhumiwa hao wanaodaiwa ‘kutumwa na afande’ ni askari wa JWTZ MT.140105 Clinton Damas, askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Lord Lema na Nickson Jackson.

Awali, watuhumiwa hao waliingia kwenye chumba cha Mahakama saa 9 alasiri lakini walirudishwa tena ili wazungumze na mawakili wanaowatetea kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi.

Aidha waandishi wa habari wamezuiwa kuingia kwenye chumba cha Mahakama wakati kesi inaendelea wala kupiga picha watuhumiwa wakiwa kwenye korido za mahakamani huku wakiambiwa wasubiri watoke nje ndiyo wawapige picha.

Bado haijajulikana idadi ya mawakili wanaowatetea wala majina yao lakini wameshafika mahakamani kwa ajili ya kuwatetea watuhumiwa hao.

Jana Jumatatu, watuhumiwa hao walipandishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo na kusomewa mashtaka mawili ya kubaka kwa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbili binti huyo.

Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Makao Makuu, Renatus Mkude alisema kesi hiyo itasikilizwa kwa siku nne mfululizo kuanza leo hadi Ijumaa, Agosti 23, 2024.


Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari na taarifa mbalimbali.