Kesi kupinga mkataba uwekezaji bandari kuanza kusikilizwa leo Mbeya

Mawakili wa kujitegemea wakiwa kwenye chumba cha Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya kwa ajili ya kuanza kusikiliza shauri la kupinga mkataba wa uwekezaji wa bandari kati ya Serikali ya Dubai na Tanzania kupitia Kampuni ya DP World. Picha na Hawa Mathias
Muktasari:
Sakata la uwekezaji bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kupitia kampuni ya DP World hatimaye limefika mahakamani leo Jumatatu Julai 3, 2023 jijini Mbeya.
Mbeya. Sakata la uwekezaji bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kupitia kampuni ya DP World hatimaye limefika mahakamani leo Jumatatu Julai 3, 2023 jijini Mbeya.
Kesi hiyo upande wa utetezi unaongozwa na wakili wa kujitegemea, Boniface Mwabukusi na Philipo Mwakilima
Kesi hiyo ilifunguliwa Juni 27, mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kupinga baadhi ya vifungu vya mkataba huo.
Kesi hiyo namba 05/2023 inawahusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Katibu wa Bunge.