Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kampuni ya UAE yafutiwa adhabu ya zabuni nchini

Dar es Salaam. Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma (PPAA) imeagiza kuondolewa kwa adhabu ya kufungiwa miaka 10 kwa Kampuni ya Al Ghurair Printing iliyokuwa imeomba zabuni ya kuchapisha karatasi za kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 hapa nchini.

Al Ghurair Printing ilifungiwa kushiriki zabuni za umma hapa nchini na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Julai mwaka huu hatua iliyosababisha wakate rufaa kwa PPAA na siku kadhaa zilizopita hukumu ilitoka kuwa wameshinda.

Awali, kampuni hiyo yenye maskani yake Dubai ilifungua kesi PPAA dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakidai kuwa walistahili kushinda zabuni hiyo iliyotolewa kwa Kampuni ya Afrika Kusini ya Ms Ren-Form CC.

Al Ghurair ilidai kuwa walistahili kushinda zabuni hiyo, lakini PPAA walihukumu kuwa walishindwa kihalali kwa kuwa nyaraka zao za zabuni zilikuwa na upungufu.

Kufungiwa kwa kampuni hiyo kunatokana na makosa yaliyofanywa wakati wa uwasilishaji wa zabuni na inadaiwa haikuwasilisha rekodi yake ya madai na kesi jambo lililosababisha NEC kuiandika PPRA kuiadhibu kampuni hiyo Julai mwaka huu.

Baada ya kuadhibiwa Al Ghurair walikata rufaa PPAA kupinga adhabu hiyo ambayo ingewazuia kutoomba zabuni za umma mpaka baada ya mwaka 2030, huku katika rufaa yao wakieleza malalamiko yao kwa NEC na PPAA.

“Mamlaka ya rufani imeona kuwa mapendekezo ya NEC kwa PPRA kuifungia kampuni hiyo yaliwasilishwa nje ya muda unaotakiwa,” ilieleza PPAA wakati wa kutoa uamuzi. Kanuni za Ununuzi wa Umma kifungu cha 94, kifungu kidogo cha kwanza kinaelekeza kuwa mtu anayetaka kuwasilisha mapendekezo ya kufungiwa kampuni kushiriki zabuni anapaswa kutoa taarifa PPRA ndani ya siku 28 tangu alipobaini kosa ambalo ni sababu ya kampuni kufungiwa.