Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jinsi ‘house girl’ anavyoharibu maisha ya mtoto wako

Muktasari:

Kabla ya miaka ya 1980, akina mama wengi walikuwa wanakaa nyumbani wakilea watoto, ni wachache sana walikuwa wameajiriwa.

Dar es Salaam. Mabadiliko ya maisha yamewafanya wazazi wengi kuwa ‘bize’ na kazi, kiasi cha kuacha majukumu ya kulea watoto kwa wafanyakazi wa ndani (ma-house girls) ambao siku hizi wengi huitwa ‘dada’.

Kabla ya miaka ya 1980, akina mama wengi walikuwa wanakaa nyumbani wakilea watoto, ni wachache sana walikuwa wameajiriwa.

Lakini, msukumo wa maendeleo, elimu, maisha na usawa wa jinsi umebadilisha hali hiyo kiasi kwamba siku hizi wanaume na wanawake wote wanafanya kazi ama zilizo rasmi au zisizo rasimi.

Hali hiyo imefanya jukumu la kuwalea watoto liachwe kwa akina ‘dada’ ambao wengi wao hutoka vijijini katika mazingira na utamaduni tofauti kuja kufanya kazi maeneo ya mjini.

Akina dada hawa ndio wamekuwa kama wazazi wa watoto hawa kwani hufanya kazi zote kuanzia kuwaamsha asubuhi, kuwaogesha, kuwapeleka shule na hata wakirudi huwapokea, huwapa chakula, huzungumza nao na huo ndio umekuwa ndio mtindo wa maisha ya kila siku.

Akina dada hawa, wengi wao wameishi maisha magumu huko vijijini na ndio maana wamekubali kufanya kazi hiyo yenye mshahara mdogo.

Kutokana na hilo ni wachache sana huwa na upendo kwa watoto, lakini hata hao wenye upendo hawawezi kujua kila kitu kuhusu malezi ya watoto. Hufanya kazi hiyo kwa sababu wana shida, lakini kiukweli hakuna mtu anayetaka kusafisha uchafu wa mtoto asiye wake.

Madhara yake huwezi kuyaona haraka, lakini watoto wanaopitia katika mikono ya akina dada hawa, huwa wanatunza kila kitu kwenye ubongo wao, liwe jambo baya au zuri.

Mtoto huyu akikua na kuwa mtu mzima na pengine ameshaoa au kuolewa, mambo yote aliyofanyiwa utotoni huanza kurudi kwenye akili yake, lakini yeye mwenyewe hawezi kutambua.

Kwa hiyo usije kushangaa mtu mzima anafanya mambo yasiyoeleweka ikiwa ni pamoja na kutowajali wazazi wake ukadhani ni bahati mbaya. Hapana, maisha ya utotoni yaliathiriwa na kupata malezi ya ‘dada’ ambayo hayakuwa na upendo, na yeye anakuwa hajui maana ya upendo, hivyo hawezi kuwajali wazazi.

Ndoa nyingi za vijana wa sasa zinavunjika, vijana wanatumia dawa za kulevya, wanapenda starehe kuliko kazi, vijana ni wavivu, wapowapo tu na wengine hawajitambui kabisa huku upeo wao wa kuelewa mambo ukiwa chini sana.

Bunge limetunga sheria kali, lakini vijana wanafungwa magerezani kila siku kwa makosa mbalimbali, kwa sababu athari waliyoipata ni kubwa na ni ngumu kuibadilisha sasa.

Kuna sababu nyingi, lakini malezi wanayoyapata kutoka kwa hawa akina ‘dada’ yamewafanya wawe hivyo. Mzazi chukua hatua sasa na ni vizuri kuwaona wataalamu wa saikolojia kwa msaada zaidi kama unahisi mtoto wako kaathirika na malezi ya akina ‘dada’.

Mwandishi wa uchambuzi huu ana shahada ya Sociology kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.