Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jela miaka 30 kwa kumnajisi mtoto wa miaka sita Njombe

Mahakama ya Wilaya ya Makete ambayo imetoa hukumu ya miaka 30 jela kwa tuhuma za ulawiti huko mkoani Njombe.

Muktasari:

  • Huyu ni Zakayo Sanga mkazi wa kijiji cha Magoye aliyekumbana na adhabu hiyo baada ya kumnajisi mtoto wa miaka sita.

Njombe. Mahakama ya hakimu mkazi Wilaya ya Makete mkoani Njombe, imemuhukumu Zakayo Sanga (35) mkazi wa kijiji cha Magoye wilayani humo kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kunajisi mtoto wa miaka sita.

Hukumu hiyo imetolewa leo Juni 5,2025 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Makete, Irvan Msacky ambapo amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo Aprili 2, 2025 ikiwa ni kinyume na kifungu cha sheria namba 130 (1) na cha (2)e na kifungo namba 131 (3) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.
Amesema amejiridhisha pasi na shaka kuwa mtuhumiwa kwa nyakati tofauti alitenda kosa hilo baada ya kusikiliza pande zote pamoja na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.

Ameeleza kuwa siku ya tukio mshtakiwa alimchukua mtoto huyo aliyekuwa akichuma maparachichi na wenzake na kwenda kumbaka huku akiwachia simu watoto wenzake na baada ya kumfanyia kitendo hicho cha kikatili, alimpa fedha na kumwambia asiseme kwa mtu.

"Hata hivyo mtoto hakusema kitendo hicho alichofanyiwa lakini walezi wake walimuona hayuko sawa na kumpeleka hospitali ndipo iligundulika kuwa amebakwa," amesema Msacky.

Awali, Wakili wa Serikali, Hosea Mwambungu ameomba mshtakiwa huyo kupewa adhabu kali ili kutoa fundisho kwa wengine kwani kitendo alichofanyiwa mtoto huyo hakikubaliki.

"Naomba Mahakama hii itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili kutoa fundisho kwa watu wengine kwani kitendo alichofanyiwa mtoto huyu hakikubaliki" amesema Mwambungu.

Mshtakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea ameomba Mahakama kumpunguzia adhabu.

"Naomba Mahakama hii inipunguzie adhabu ya kosa nililofanya kwani sikudhamiria" amesema Sanga.

Akizungumzia hukumu hiyo, Ofisa ustawi wa jamii wilaya ya Makete, Maiko Bazili amesema matukio ya aina hiyo ni miongoni mwa wanayokutana nayo, hivyo jamii inapaswa kuwa makini zaidi.

“Kila mwananchi ana haki ya kutoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika pindi mtoto anapofanyiwa ukatili, kwani mtuhumiwa asiposhughulikiwa anaweza kutenda kosa la aina hiyo kwa mtoto mwingine,” amesema Bazili.

Ametoa wito kwa wazazi na walezi wilayani humo kuwalinda watoto katika kipindi watakachokuwa likizo baada ya shule kufungwa.