Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haya hapa masharti kupata Samia Scholarship

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda akizungumza katika mkutano wa wadau wa elimu wa mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 na mitaala ya elimu jijini Dodoma. Picha na  Merciful Munuo

Muktasari:

Serikali imetangaza masharti saba kwa wanafunzi watakaoomba kunufaika na ufadhili (Samia Scholarship), ikiwemo kuhakikisha kuwa kiwango cha ufaulu hakishuki chini ya GPA 3.8 katika mwaka wa masomo baada ya kupewa ufadhili huo.

Dodoma. Serikali imetangaza masharti saba kwa wanafunzi watakaoomba kunufaika na ufadhili (Samia Scholarship), ikiwemo kuhakikisha kuwa kiwango cha ufaulu hakishuki chini ya GPA 3.8 katika mwaka wa masomo baada ya kupewa ufadhili huo.

Masharti mengine ni mnufaika kutoruhusiwa kuahirisha masomo isipokuwa kwa sababu za kiafya, kuthibitishwa na chuo husika, kuwa na akaunti ya benki kwa ajili ya kuingiziwa fedha, kusoma na kuelewa mkataba wa makubaliano ya ufadhili wa masomo kati yake na Wizara ya Elimu kabla ya kuusaini na mnufaika kujisajili katika mfumo wa usimamizi wa wanafunzi.

Akizungumza juzi katika mkutano wa wadau wa elimu kujadili mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 na mitalaa ya elimu pamoja na kufungua dirisha kwa ajili ya ufadhili huo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda alisema ufadhili huo utahusisha ada ya mafunzo, posho ya chakula, malazi, vitabu, mahitaji maalumu ya vitivo, vifaa saidizi kwa wenye mahitaji maalumu na bima ya afya.

Alisema majina ya wanafunzi waliopata ufaulu wa juu kwenye masomo ya Sayansi katika mitihani ya kidato cha sita, yalianza kutangazwa jana katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).

“Wanafunzi watakaofadhiliwa, watagharamiwa kati ya miaka mitatu hadi mitano kulingana na programu husika walizodahiliwa. Hakuna kushawishi kama hujafaulu usipige simu,” alisema.


Mgawanyo wa wanafunzi

Profesa Mkenda alisema uwiano wa kijinsia wa wanufaika 640 wa Samia Scholarship ni kwa wasichana 244 na wavulana 396 ikijumuisha Tanzania nzima.

“Wanafunzi kutoka shule za Serikali ni 396 sawa na asilimia 62 na kutoka shule binafsi ni 244 sawa na asilimia 38. Wanafunzi wenye kiwango cha alama tatu ni sita (sawa na asilimia 9).

Profesa Mkenda alisema idadi kubwa ya wanufaika wa Samia Scholarship na asilimia katika mabano ni Tabora Boys ambayo imetoa wanafunzi 79 (12), St Mary’s Mazinde Juu 51 (8), Mzumbe 46 (7), Tabora Girls 39 (6) na Kisimili 31 (5).

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein, alisema utaratibu huo utasaidia kuhamasisha wanafunzi kujitokeza kusoma masomo ya sayansi.