Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haya hapa majina na shule walizochaguliwa kujiunga wanafunzi wa kidato cha kwanza 2024

Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa akitangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za kutwa na bweni za Sekondari nchini leo jijini Mwanza. Picha na Mgongo Kaitira

Mwanza. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa ametangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za Serikali nchini mwaka wa masomo 2024.

Angalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza https://shorturl.at/fTW49

Majina hayo yanajumuisha ya wanafunzi waliochaguliwa kwenda kusoma shule za sekondari za bweni, vipaji maalum na kutwa za Serikali.

Mchengerwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa, wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga shule za kutwa wanaripoti shuleni ifikapo Januari 8, 2024 huku waliochaguliwa shule za bweni wakitakiwa kuripoti ifikapo Januari 6, 2024.

Waziri huyo amesema hayo leo Jumapili, Desemba 17, 2023, jijini Mwanza alipozungumza na waandishi wa habari.