Matokeo ya darasa la saba 2023 haya hapa

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (Necta). Dk Said Mohammed akitangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba ya mwaka 2023 jijini Dar es salaam, Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji Angela Kitali. Picha na Said Khamis
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba uliofanyika Septemba 13-14, 2023.
Matokeo hayo yametangazwa leo, Alhamisi Novemba 23, 2023 na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Mohammed.
Kwa mujibu wa Dk Mohammed, wanafunzi 360 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani yote au idadi kubwa ya masomo, watarudia tena mwaka 2024 huku wakitangaza kufuta matokeo ya wanafunzi 31 kwa kufanya udanganyifu.