Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gari lililokuwa limebeba wanafunzi lakamatwa na mirungi

Muktasari:

  • Watu watatu ambao ni wafanyakazi wa basi la kampuni ya Extra luxury, wanashikiliwa mkoani Kilimanjaro baada ya gari hilo lililokuwa limebeba wanafunzi kukamatwa likiwa na dawa za kulevya aina ya mirungi wilayani Same.

Same. Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, linawashikilia wafanyakazi watatu wa basi la kampuni ya Extra Luxury kwa kukutwa na bunda 316 na kilo 55 za mirungi zilizokuwa ndani ya gari hilo lililobeba wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha Science waliokuwa wanakwenda likizo.

 Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Simon Maigwa amesema gari  hilo lilikamatwa  Desemba 6, mwaka huu, saa nne na nusu asubuhi, katika eneo la majengo mapya, Hedaru, Wilaya ya Same likitokea mkoani Arusha kwenda Dar es Salaam.

Kamanda Maigwa amesema baada ya polisi waliokuwa doria kupata taarifa za gari hilo kuwa limebeba dawa hizo za kulevya lilipofika eneo la Majengo, wilayani Same  walifanya upekuzi ndani ya gari hilo na kwenye buti walikuta dawa hizo za kulevya.

"Baada ya kukamata hili gari, tulifanya upekuzi,  kwenye buti tulikuta gari limebeba mirungi bunda 316 na kilo 50 za mirungi, kwa hiyo  tumewakamata watu watatu  ambao ndio wahusika wa hilo gari," amesema Kamanda Maigwa.

"Kwa kuwa gari hilo lilikuwa limebeba wanafunzi liliruhusiwa lipeleke wanafunzi kwenda Dar es Salaam lakini likarudi tena na watu, kwa hiyo gari liko kituoni mpaka sasa," amesema.

Kamanda Maigwa amesema watuhumiwa hao watatu ambao ni wafanyakazi wa kampuni hiyo, watafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Alipotafutwa mmiliki wa gari hilo, Hermet Massawe amesema taarifa hizo hana na kwamba aachwe afuatilie.