Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gambo alia gharama za bando

Mbunge wa Arusha Mjini (CCM) Mrisho Gambo

Muktasari:

  • Bei ya ‘mabando’ ya internet, imemuibua Mbunge wa Arusha Mjini (CCM) Mrisho Gambo ambaye ametaka Serikali kuangalia bila kulinganisha na nchi nyingine duniani.

Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo amewataka mawaziri kuangalia upya gharama za mabando ya simu ili kuwapunguzia gharama wananchi.

Gambo ameyasema hayo leo Jumatano Juni 21, 2023 wakati akichangia hali ya uchumi, Mpango wa Maendeleo wa Taifa na bajeti ya mwaka 2023/24.

“Gharama za bando zimepanda sana majibu tunayopewa hayaendani na hali halisi unaambiwa sijui zima ‘App’ hii, unaambiwa sijui fanya hivi hicho ni kitu kimoja kitatupunguzia matumizi,” amehoji Gambo.

Amesema mwaka 2020 ukinunua data za Sh15, 000 unapata GB 10 leo hii unapata kati ya GB7.2 hadi GB 7.38.

Amesema makampuni hayo hayajaongeza bei lakini wamepunguza bando na hivyo kwa namna nyingine wameongeza bei.

Amefafanua kuwa wakati huo wastani wa GB moja ulikuwa Sh1, 500 lakini leo hii unapata kwa Sh2, 054

“Ndio maana watoto mashuleni ukiwawekea bando kidogo tu limeisha, inaongeza gharama kwa Watanzania, inapunguza ubunifu ni vizuri mkaliangalia vizuri.

“Na tusiambiwe kuwa mbona kwa gharama hizi ni ndogo, ile ni dunia na Tanzania ni Tanzania, tuzungumza Tanzania hatuwezi kufanana na nchi nyingine duniani,” amesema.