Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Familia ya Dk Tulia yasimulia ilivyopokea ushindi IPU

Rais wa 31 wa Umoja wa Mabunge ya  Dunia (IPU) na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali wakiwepo wanafamilia, nyumbani kwao katika kijiji cha Bulyaga Kata ya Mabonde Wilaya ya Rungwe mara baada ya mapokezi na kufanya ibada ya kumuombea. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Imeelezwa kuwa hawakutarajia kama leo angefikia hatua hiyo kutokana na maisha aliyotapitia kuuza vitumbua,vibama nyanya kwenye genge la dada yake.

Rungwe. Mamia ya wananchi wa rika tofauti wamejitokeza nyumbani kwa wazazi wa Rais wa 31 wa Umoja wa Mabunge ya Dunia (IPU) katika kijiji cha Bulyaga Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya huku familia yake ikieleza namna ilivyopokea ushindi wa mtoto wao kuwa Rais wa IPU.

Licha ya familia kumuelezea Dk Tulia ambaye pia ni Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini, viongozi mbalimbali wa CCM wakiwamo wabunge wametumia fursa hiyo kuelezea hisia zao.

Awali akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumapili Novemba 12, 2023 katika Kijii cha Bulyaga ,Dada wa Dk Tulia, Odima Ackson amesema malezi aliyopitia kama familia hawakutarajia kama angefikia hatua hiyo kubwa Duniani.

“Mimi ni Dada yake Dk Tulia nimemlea maisha ya chini sana na muda mwingi baada ya masomo alikuwa akinisaidia kuuza vitumbua, vibama na nyanya kwenye genge langu.

“Tangu utoto wake alikuwa ni msikivu sana na hata nikisafiri nilikuwa nina uhakika biashara itakwenda vizuri kwa kweli, kama familia hatukutarajia kabisa siku tuliyopata taarifa tulilia kwa furaha,”amesema.

Amesema kuwa kama familia wanatambua ni wakati wa Mungu na ni kudra zake.

“Kwa kweli leo hii hatukutarajia familia yetu kuleta kiongozi mkubwa Duniani, ukoo wa Ackson Mwansansu tumepokea baraka za Mungu kwa mdogo wetu kipenzi Dk Tulia,”amesema.

Odima amesema kuwa hawawezi kupingana na wakati wa Mungu kikubwa wanaomba wanambeya waendelee kumuombea katika nafasi hiyo kubwa kwa Dunia.


Matarajio yao

Ni kuona anaendeleza upendo, mshikamano, utii kwa watu wote na pia kama familia wanaendelea kufanya maombi katika nafasi aliyopewa na Mungu.

“Neema ya Mungu itamuongoza na maombi ya Watanzania, macho yetu na matarajio yetu akaendelee kuwa Nuru ya kweli kwa dunia,”amesema.

Elimu

Amesema Dk Tulia alihitimu elimu yake ya msingi katika Kata ya Mabonde iliyopo wilayani rungwe 1994 huku elimu ya Sekondari alisoma Shule ya wasichana Roleza iliyopo jijini Mbeya na baada ya aliendelea na elimu ya kidato cha tano na sita Zanaki Sekondari jijini Dar es Salaam.

Kauli za Wabunge

Mbunge wa Makete, Festo Sanga amesema kuwa nafasi ya mwanamke aliyopata Dk Tulia ni wakati wake na kwamba wananchi mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wamtumie kama tunu kwani ni wakati wa vita katika kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.

“Sasa tunakwenda kutoa elimu kwa wanawake kutambua kuwa demokrasia huru ya wanawake kushika nafasi za juu, pia  tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuona Dk Tulia kufaa kuwa  Rais wa 31 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Naye mwakilishi wa wabunge wanawake Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Suma Fyandomo amesema Dk Tulia amewaheshimisha wanawake na wabunge na kuleta taswira ya heshima kidunia.

“Tuliishi naye ni mtoto wetu katika makuzi yake hajawahi kumdharau mtu,amekuwa akishirikiana vyema na wananchi,kujitoa kuwasaidia hakika ni wakati wake Mungu umefika kutuletea kiongozi wa dunia,”amesema.