Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Nchimbi aongoza kikao kujadili masuala ya Muungano, hoja ya sukari yamalizwa

Muktasari:

  • Aprili 26, 1964, Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuzaa Tanzania. Kesho Jumapili Aprili 26, miaka 62 ya Muungano huo huku kero mbalimbali za Muungano huo zikiwa zimetatuliwa.

Zanzibar. Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Emmanuel Nchimbi leo Jumamosi, Aprili 25, 2026 ameongoza kikao cha kamati ya pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kushughulikia masuala ya Muungano kilichofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar.

Dk Nchimbi amewapongeza viongozi na wataalamu wote walioshiriki katika kikao hicho kwa jitihada walizofanya wakati wa maandalizi na majadiliano.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Emmanuel Nchimbi (katikati) akiongoza kikao cha kamati ya pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kushughulikia masuala ya Muungano kilichofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar.

Katika kikao hicho hoja ya uingizaji wa sukari kutoka Zanzibar katika Soko la Tanzania Bara imeridhiwa na kuondolewa katika orodha ya hoja za Muungano, ambapo imeshuhudiwa kusainiwa kwa hati ya makubaliano ya kuondoa hoja hiyo katika orodha ya Hoja za Muungano ambayo ni miongoni mwa hoja nne za Muungano zilizokuwa zimesalia.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),  Mhandisi Hamad Masauni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili ya Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi), Hamza Hassan Juma.

Viongozi wakiwa katika kikao cha kamati ya pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kushughulikia masuala ya Muungano kilichofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar.

Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Katibu Mkuu Kiongozi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Moses Kusiluka, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Saleh Juma Mussa, makatibu wakuu, wakuu wa taasisi pamoja na wataalamu mbalimbali.