Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwigulu: Jadilini sheria zinapotungwa, sio zinapotekelezwa

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba akijibu swali bungeni katika kikao cha 27 cha mkutano wa Bunge la Bajeti, jijini Dodoma leo Mei 16, 2024. Picha na Merciful Munuo

Muktasari:

 Awashauri wabunge kujadili wakati sheria ikutungwa na si wakati wa utekelezaji.

Dodoma. Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba, amewataka Watanzania kujenga utaratibu wa kujadili sheria zinapotungwa na si zinapotekelezwa.

Amesema hayo leo Mei 16, 2024 akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mbozi, George Mwenisongole, aliyehoji iwapo Serikali haioni haja ya kuondoa mashine za kieletroniki (EFD) kwa vyama vya ushirika nchini vinavyouza kwa mwaka mara moja.

Dk Mwigulu ametaka kutengenezwa utaratibu wa kujadili sheria inapotungwa na si wakati wa utekelezaji baada ya kutungwa.

“Hili ni jambo la kisheria, mwezi ujao tutajadiliana tena mambo yanayohusu hatua za kikodi, kama tunaona kuna sheria haifai, Bunge lako tukufu liifute. Lakini sheria zozote zinazotungwa tusijadili kuhusu utekelezaji wake,” amesema.

Amesema sheria yoyote ya nchi ikishatungwa, inatakiwa kutekelezwa na kusimamiwa utekelezaji wake.

“Hatuwezi kumtoza mtu wa kima cha chini anayepokea milioni tatu kwa mwaka halafu tukamuacha anayepokea Sh100 milioni kwa mwaka,” amesema.

Dk Mwigulu amesema si haki kuchukua kodi ya mwalimu wa shule za msingi kwa msingi kuwa kukusanya kwake hakuleti kero lakini akaachwa tajiri kwa misingi kuwa ukusanyaji wake ni kero.

Katika swali la msingi mbunge huyo amehoji ni kwa nini Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inalazimisha vyama vya msingi vya ushirika kutumia EFD wakati hawafanyi biashara na mauzo yao ni mara moja kwa mwaka.

Dk Mwigulu amesema ukusanyaji kodi unafanyika chini ya kifungu namba 36 (1) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya mwaka 2015.

Amesema kifungu hicho kinaelekeza kuwa: “Mtu yeyote anayesambaza bidhaa, kutoa huduma au kupokea malipo kuhusu bidhaa au huduma anazosambaza anatakiwa kwa mujibu wa sheria kutoa risiti za mashine za kieletroniki kulingana na kiasi cha fedha alichopokea kutokana na bidhaa au huduma aliyotoa.”

Amesema taratibu za kikodi zimebainisha mfanyabiashara yeyote mwenye mauzo ghafi yenye kiasi cha Sh11 milioni na kuendelea kwa mwaka anapaswa kutumia mashine za EFD.

“Sharti hili la kisheria linahusisha walipakodi wote wanaofanya biashara mara nyingi au mara moja kwa mwaka,” amesema.

Waziri Mwigulu amesema lengo la Serikali kuanzisha matumizi ya mashine za EFD ni kuhamasisha na kujenga utamaduni wa kutunza kumbukumbu za biashara.

Amesema mashine ya EFD ni kati ya vifaa ambavyo humsaidia mfanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara kwa muda mrefu na kwa upande mwingine, huisaidia Serikali kutambua mauzo na kutoza kodi stahiki pale inapopaswa kufanya hivyo.

Amesema EFD inahakikisha dhana ya uwazi inasimamiwa kikamilifu.