Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mpango awaweka mtegoni manaibu watatu

Makamu wa Rais Dk Philip Mpango akipita kwenye daraja la dharura lililotengenezwa kwa nyaya.

Kondoa. Makamu wa Rais Dk Philip Mpango ametoa maagizo kwa naibu  mawaziri wanne ya kushughulikia matatizo ya wananchi katika Halmashauri ya Kondoa Mji.

Dk Mpango ambaye yupo kwenye ziara mkoani Dodoma ametoa maagizo hayo leo Jumatano Agosti 21, 2024 alipozungumza na wananchi wa Kijiji cha Hurui wakati akizindua daraja ambalo linaunganisha wilaya mbili za Babati mkoani Manyara na Kondoa (Dodoma). Kabla ya ujenzi wa daraja hilo wananchi walikuwa wakitumia daraja la dharura lililotengenezwa kwa nyaya.

Daraja hilo awali lilisombwa na maji na kusababisha shida kwa wananchi ikiwamo watoto kushindwa kwenda shule na huduma nyingine za kijamii kama hospitali na mahitaji ya nyumbani.

Ujenzi wa daraja la Hurui umegharimu Sh1.6 bilioni na linatarajiwa kuwa kiungo muhimu na kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kwa kurejesha mawasiliano kati ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma na Wilaya ya Babati mkoani Manyara.

Daraja hilo lenye urefu wa mita 30 limejengwa kwenye Barabara ya Ntundwa – Mkunduru -Hurui yenye urefu wa kilomita 46.4.  Mradi huo umehusisha uboreshaji wa kilomita nane za barabara kwa kiwango cha changarawe.

Katika maagizo yake kwa Naibu Waziri wa Nishati,  Judith Kapinga kuhakikisha wananchi kwenye kijiji hicho wanawawekewa umeme kwenye nyumba zao.

Dk Mpango alifikia hatua hiyo baada ya kuwauliza wananchi kama wana umeme na walimjibu, umeme upo barabarani lakini siyo kwenye nyumba zao.

Pia, Dk Mpango amemuagiza Naibu Waziri wa Maji, mhandisi Kundo Mathew ahakikishe itakapofika Oktoba 30 mwaka huu maji yanapatikana kwenye kijiji hicho na vingine vitano.

"Nataka ujifunge hapa ikifika Oktoba 30 uje hapa uhakikishe maji yanatoka kwa kumtwisha ndoo ya mama kichwani na upige na picha ikiwemo video uniletee nione" amesema Dk Mpango.

Pia, Dk Mpango amemuagiza Naibu Waziri wa Ardhi, Geoffrey Pinda kuwa  katika kipindi cha Bunge aende na mbunge wa Kondoa Vijijini, Dk Ashatu Kijaju ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mazingira kijijini hapo kushughulikia tatizo la mgogoro wa ardhi.

Naibu mawaziri hao wako kwenye ziara ya Dk Mpango mkoani humo.

Pia, Dk Mpango ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Daraja la mto Hurui lililopo kata ya Kikore Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, huku akiwahimiza wananchi wa kata ya hiyo   na watumiaji wa daraja hilo kutunza miundombinu iliyojengwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na baadaye.

Pia amewaagiza Wakala wa Barabara Mijini na Vijiji (Tarura) kufanya ukarabati wa Barabara ya Ntundwa – Hurui ya wilayani Kondoa, ili kuwarahisishia wananchi shughuli za kiuchumi ikiwemo usafirishaji mazao.