Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Biteko ataka wachimbaji madini wanawake waungwe mkono

Waziri wa Madini, Dk Dotto Biteko akizungumza na wananchi (hawapo pichani) alipotembelea mchimbaji mdogo wa Mgodi wa Madini aina ya Rhodorite iliyopo Kijiji Cha Ng'alo kata ya Lubeho Wilayani Gairo. Picha na Picha Lilian Lucas.

Muktasari:

Waziri wa Madini, Dk Dotto Biteko amesema uchimbaji wa madini kwa miaka mingi ulikuwa ikifanywa na wanaume zaidi kuliko wanawake na kwamba tafiti za Wizara zilizopo zinaonyesha kati ya watu 100 wanawake saba pekee ndio wachimbaji.

Morogoro. Waziri wa Madini, Dk Dotto Biteko amesema uchimbaji wa madini kwa miaka mingi ulikuwa ikifanywa na wanaume zaidi kuliko wanawake na kwamba tafiti za Wizara zilizopo zinaonyesha kati ya watu 100 wanawake saba pekee ndio wachimbaji.

Pia, ameitaka jamii kuwaunga mkono na kuwatia moyo wanawake wanaojitokeza katika shughuli hiyo ya uchimbaji madini.

Dk Biteko amesema hayo Januari 6, 2021 alipomtembelea mchimbaji wa madini ya vito aina ya Rhodorite katika kijiji cha Ng’alo kata ya Lubeho Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

Dk Biteko amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwa Wizara ya Madini kuhakikisha changamoto zilizopo kwa wachimbaji zitatuliwe.

“Wanaweke wengi wako kwenye kutoa huduma za kupika chakula, kuuza maji na soda hawa wanawake waliojitokeza akiwemo huyu tunapaswa kuwaunga mkono na kuwatafutia masoko,” amsema na kuongeza

“Kumkuta mwanamke anachimba kama alivyo mchimbaji Fatuma ni wachache ila tunawahamasisha wajitokeze kwenye sekata hii,”amesema.

Amesema soko la madini ya vito Duniani kwa sasa limeyumba baada ya kutokea kwa Uviko 19.

Waziri huyo wa madini amesema kwa sasa madini ya vito yamekuwa yakikosa soko lakini Serikali inaendelea kutafuta soko ili kuondoa changamoto iliyopo na kuondoa migongano baina ya wachimbaji na wafanyakazi wao.

“Tunahangaika kutafuta masoko na wanunuzi wakubwa wa madini hayo ni Wachina na Wathailand, sisi tutaanza kuwatangazia fursa hii waje wanunue ili wawee kunufaika,”amesema.

Mmiliki wa mgodi huo wa madini ya Rhodorite, Fatuma Hassan amezungumzia sula la changamoto ya soko la madini hayo, vitendea kazi, ukosefu wa mitaji, kugawana kwa asilimia baina ya mchimbaji na wafanyakazi, pamoja na uzalishaji mdogo.


Amesema awali soko kuu lilikuwa ni kutoka nchini Chini na Thailand na kwamba tangu kuanza kwa uchimbaji mwezi Mei, 2021 amekuwa akichimba na kuhifadhi bila kupata soko.

Ofisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Emmanuel Shija amesema masoko yanaendana na mahitaji ya kila mwezi, hivyo mkoa wanaendelea kuwasimamia na kutoa elimu kwa wachimbaji wote katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Mwenyekiti wa Chama Cha wachimbaji Mkoa wa Morogoro, Dk Omary Mzeru amesema miongoni mwa changamoto zilizopo ni ukosefu wa soko la madini ya viwandani hasa ukizingatia mkoa wa Morogoro una madini ya viwandani.

"Tatizo la kukosa soko linawafanya kukosa fursa ya kujikwamua kimaisha na kitokuongezeka kwa Pato la Taifa” amesema

Ameipongeza Benki ya NMB kwa namna inavyoonyesha nia ya kusaidia wachimbaji kwa kuwapatia mikopo kwa dhamana ya leseji zao zinazoonyesha Kuwepo kwa akiba ya madini kwenye Ardhi," amesema.