Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diwani aliyekuwa mbaroni kwa tuhuma za mauaji afariki

Muktasari:

  • Wananchi Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wamesikitishwa na kifo cha Diwani wa Kata ya Buzilazoga Devid Shilinde aliyepoteza maisha wakati anapatiwa matibabu katika Hospitari ya Rufaa Bugando alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kisukari.

Mwanza. Diwani wa Buzilasoga wilayani Sengerema mkoani Mwanza (CCM), David Shilinde amefariki dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando jijini Mwanza.

Shilinde ambaye alitumikia nafasi hiyo ya udiwani kwa tiketi ya CCM kwa miaka 13, alikuwa katika mahabusu ya Polisi kutokana na kutuhumiwa kuhusika kwenye mauaji ya Getruda Dotto, mauaji yaliyotokea Novemba 5,2022 kwenye Kitongiji cha Ikoni.

Kifo cha diwani huyo kimethibitishwa na mtoto wake, Fabian Shilinde ambaye ameieleza Mwananchi kuwa baba yake alifariki usiku wa kuamkia Jumatano, Septemba 27, mwaka huu akipatiwa matibabu hospitali ya Bugando.

Amesema kabla ya kutiwa mbaroni kwa tuhuma za mauaji, baba yake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kisukari ambacho kwa mujibu wa madaktari ndicho kimepelekea kifo chake.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashuari ya Sengerema, Makoye Sengerema amesema baraza la Madiwani la Sengerema limepata pigo kutokana na kifo cha Shilinde na kusema diwani huyo alikuwa mstari wa mbele kushauri na kusimama vema miradi ya maendeleo kwenye kata yake.

"Sisi kama madiwani tutaendelea kuyaenzi yote aliyotuachia mwenzetu alionyesha moyo wa upendo kuwatumia wananchi wake na Madiwani kwa ujumla,” amesema Sengerema.

Magilu Magembe ni mkwe wa marehemu Devid Shilinde amesema kifo cha baba mkwe wake ni pigo kwake kutokana ushauri wake kwenye familia yake aliokuwa akiutoa kudumisha ndoa ya watoto wao.

Mmoja wa rafiki wa karibu wa marehemu, Samsoni Deusi ambaye ni katibu wa CCM kata ya Buzilazoga ameseme kifo cha diwani wake nipengo kubwa kwake na chama chake na wananchi wa Kata ya Buzilasoga.

Kwa upande wake Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu amesema kifo cha Diwani Shilinde ni pigo kwa CCM na wananchi wa Kata ya Buzilazoga hivyo watayaenzi mema yote aliyowaachia ikiwemo kusimamia vyema miradi ya maendeleo kwenye kata ya Buzilazoga na ndiyo alama aliyowaachia.

Katibu wa CCM Wilaya ya Sengerema, Waridi Mngumi amesema kifo cha diwani huyo ni pigo kwa CCM kutokana na uchapakazi wake na mdiwani wenzake ambao wako timu moja katika kutekeleza Ilani ya chama hivyo kuondoka kwake nipigo ambalo haliwezi kuzibika kwa haraka na ametoa wito kwa familia na WanaCCM kwa ujumla kushikamana katika kipindi hiki kigumu baada ya kuondokewa na mpendwa wao.