Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dereva wa Tanesco aliyefariki ajalini alistaafu mwaka jana

Muktasari:

  • Ajali hiyo ilitokea Aprili 13, 2025 eneo la Nyatwali, wilayani Bunda Mkoa wa Mara, wakati mkurugenzi huyo na dereva wake Haule, walipokuwa wakitokea jijini Mwanza

Kibaha/Musoma. Imeelezwa kuwa dereva wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Muhajiri Haule, aliyepoteza maisha katika ajali ya gari iliyosababisha pia kifo cha Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Gissima Nyamo-Hanga, alikuwa amestaafu utumishi wa umma tangu mwaka jana.

Ajali hiyo ilitokea Aprili 13, 2025 eneo la Nyatwali, wilayani Bunda Mkoa wa Mara, wakati mkurugenzi huyo na dereva wake Haule, walipokuwa wakitokea jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, chanzo cha ajali hiyo dereva wa gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser, kumkwepa mwendesha baiskeli barabarani.

Hali hiyo ilisababisha dereva wa gari hilo kupoteza mwelekeo na kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitokea mbele.

Wakati Haule akizikwa Kibaha mkoani Pwani leo, mwili wa Nyamo-Hanga unatarajiwa kuzikwakesho nyumbaniMigungani mjini Bunda.

Akisoma wasifu wa marehemu Haule leo, Aprili 15, 2025 kabla ya mazishi yaliyofanyika nyumbani kwao Visiga, wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani, mmoja wa wanafamilia, Amiry Lwambano, amesema marehemu aliendelea kufanya kazi Tanesco kwa mkataba maalumu baada ya kustaafu, kutokana na utendaji wake bora wa kutekeleza majukumu.

Lwambano amesema Haule alikuwa mtumishi mtiifu, mchapakazi na aliyeaminiwa sana na uongozi wa shirika, hali iliyosababisha kuongezewa mkataba wa kazi ili kuendelea kutoa huduma kwa taasisi hiyo muhimu.

"Marehemu alistaafu mwaka jana mwezi wa nane, lakini kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi ofisi ilimuongezea mkataba wa miaka miwili akaendelea na kazi," amesema Lwambano.

Aliyekuwa dereva wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Hajiri Haule enzi za uhai wake.

Amesema katika utumishi, Haule ndiye dereva wa kwanza kuendesha wakurugenzi watano mfululizo  wa shirika hilo na aliajiriwa mwaka 1988.

"Siku anastaafu ndio ilikuwa siku yake ya kuzaliwa na aliniita tukaja kufanya sherehe hapa nyumbani kwake na siku iliyofuata akapewa barua ya kuendelea na kazi kwa mkataba wa miaka miwili,"amesema Lwambano.

Amesema anashukuru uongozi wa Tanesco kutokana na ushirikiano waliouonesha kwa kutoa huduma zote muhimu ikiwamo chakula viti na maturubai.

"Vyote unavyoviona hapa gharama zote ni Tanesco, hivyo tunawashukuru sana kwa kuonesha utu katika tatizo hili linalotukabili," amesema Lwambano.

Mmoja wa ndugu wa marehemu Hassan Hassan amesema taarifa za ajali ya ndugu yao walizipata saa nane usiku baada ya kupigiwa simu.

"Tulipata taarifa ya ajali kwa njia ya simu tukaambiwa kuna ajali imetokea hapa na wakatuuliza kuwa humo kwenye mabegi yao wamekuta vitambulisho vyenye majina yao," amesema Hassan.

Meneje wa Tanesco Mkoa wa Pwani, Mahawa Mkaka amesema wamepokea kwa masikitiko kifo cha dereva huyo.

"Hatuna namna tumepokea kwa uchungu msiba huu mkubwa kwetu,"amesema Mkaka.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema marehemu watamkumbuka kwa mengi, ikiwamo kuwasaidia kufikisha huduma ya umeme mtaani kwao.

"Tulijiitahidi sana kuhangaikia kuvuta umeme huku ikawa ngumu lakini huyu marehemu alifanya jitihada umeme ukaletwa hapa,"amesema Theresia Majaga.

Kutoka Bunda, mazishi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco,  Gissima Nyamo-Hanga yanatarajiwa kufanyika kesho nyumbani kwao eneo la Migungani mjini Bunda ukitokea hospitalini.

Kaka wa marehemu Robert Nyamo-Hanga amesema baada ya mwili kuwasili kutakuwa na shughuli  mbalimbali  ikiwamo ibada na maombolezo.

"Kama unavyojua, kesho ndugu yetu atapumzishwa katika nyumba yake ya milele kwa hiyo kabla ya mazishi mwili utawasili leo jioni na utalala hapa hapa nyumbani tayari kwa taratibu zingine za kesho," amesema.