Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dawa watumishi kuvujisha siri za Serikali yaandaliwa

Muktasari:

Serikali imeandaa mtalaa  wa mafunzo elekezi kwa mawakili na wanasheria wa umma nchini Tanzania ili kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo uvujaji wa siri za Serikali

 


Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema kukamilika kwa mtalaa wa  mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya katika utumishi wa umma itakuwa mwarobaini wa matatizo mbalimbali ikiwemo kuvuja kwa siri za Serikali.

Akizungumza leo Alhamisi Novemba 29, 2018 mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Utumishi na Umma katika Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Mathew Kirama amesema wanasheria wapya katika mtumishi wa umma kabla ya kukabidhiwa majukumu yake atapikwa na kupikika ipasavyo.

Amesema ofisi yake itafarijika kuona kila mwanasheria aliyeajiriwa serikalini anafahamu ipasavyo majukumu, wajibu, muundo wa Serikali, maadili, nidhamu na utunzaji wa siri.

“Mambo haya ni nguzo kubwa katika utumishi wa umma. Katika miaka ya hivi karibuni imekuwa rahisi kwa mwanasheria kuajiriwa serikalini bila kujua miiko au taratibu za utumishi wa umma,” amesema.

“Hii imesababisha baadhi ya wanasheria kutojua wajibu wao kwa Serikali wanayoitumikia, wakati mwingine imesababisha kuvuja kwa siri za Serikali.”

Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Jaji Paul Kihwelo amesema lengo la mkutano huo ni kupitia mtalaa wa mafunzo elekezi kwa mawakili na wanasheria wa sekta na kutoa maoni.

Amesema ingawa mafunzo yanafanyika kwa wanasheria na majaji walioko kwenye utumishi wa umma haijawahi kuwepo na mtaala kama huo unaoandaliwa.