Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dawa 127 za asili zasajiliwa, ipo ya Kisukari

Dismas Tullo ambaye ni Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) akizungumza na Mwananchi juu ya mimea waliyoifanyia tafiti na kutengeneza dawa ya kisukari. Picha na Aurea Simtowe

Muktasari:

  • Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala limesema hadi Juni 2024 dawa 127 zimesajiliwa na kati ya hizo hakuna ya kutibu Ukimwi wala figo iliyopewa usajili.

Dar es Salaam. Wakati mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) akiwa amekamilisha utafiti wake na kutengeneza dawa ya kisukari inayotumia mitishamba, Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala limesema hadi Juni 2024 dawa 127 zimesajiliwa.

Mbali na kusajiliwa kwa dawa hizo, baraza limeweka wazi kuwa hakuna dawa ya figo wala Ukimwi iliyosajiliwa kwa sababu sheria inalikataza licha ya kuwapo kwa baadhi ya watu wanaodai wanazo dawa hizo.

Mwananchi, ilikutana na Dismas Tullo ambaye ni mhadhiri katika ndaki ya kemia ya Udom, wakati wa maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) na kufanya naye mahojiano juu ya dawa hiyo ya kisukari.

Akiwa ameshirikiana na wenzie watano katika kufanikisha utafiti huo amesema, mimea iliyotumika inapatikana katika mazingira ya Tanzania na mmoja ukitoka India.

Amesema baada ya kufanyika kwa tafiti, mimea hiyo ilipochanganywa na kufanyiwa majaribio ilionyesha kuwa na ufanisi sawa na dawa zinazotoka viwandani.

“Kwa sasa tupo katika hatua za kuisajili katika Baraza la Tiba Asilia na Tiba Mbadala baada ya kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali,” amesema Tullo.

Amesema dawa hizo zinazopotumiwa na mtu mwenye aina ya pili kisukari, sukari yake inakuwa katika kiwango kinachotakiwa bila kujali kama ilikuwa juu au chini.

Kaimu Msajili Baraza la tiba Asili na Tiba Mbadala, Martin Magogwa amesema tangu mwaka 2010 hadi Juni 2024 jumla ya dawa 127 zimesajiliwa na baraza hilo zikiwemo za kisukari na shinikizo la damu.

“Ila dawa za kutibu magonjwa kama figo na Ukimwi hazisajiliwi kwa sababu sheria inasema Serikali ndiyo mtoaji wa dawa hizo na mpaka sasa hakuna mganga ambaye amethibitishwa na baraza kuwa anaweza kutoa dawa ya kutibu Ukimwi,” amesema Magogwa.

Amesema baadhi ya dawa zilizosajiliwa zinauzwa katika maduka ya dawa muhimu za binadamu na nyingine zinatumika katika hospitali mbalimbali za Serikali za rufaa za mikoa kupitia huduma jumuishi za tiba asili za kisasa.

“Mpaka sasa tunazo hospitali saba za rufaa za mikoa zinatumia dawa za tiba asili ambazo zimesajiliwa na baraza hili,” amesema Magogwa.