Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Daraja la Mbwemkuru latitia upande mmoja

Eneo la daraja la mto Mbwemkuru linaloukanisha wilaya za Kilwa na Lindi  lililotitia upate mmoja  baada ya mto kuhama kwenye njia yake ya asili na kuharibu kingo za daraja hilo. Picha na Frank Said

Muktasari:

  • Barabara imechimbika, ingawa mvua hainyeshi maeneo hayo, inaelezwa maji yamefurika katika daraja yanayoshuka kutoka maeneo mengine inakonyesha mvua.

Lindi. Boksi la Kalavati namba moja kabla ya kufika kwenye daraja kubwa la Mbwemkuru lililopo mpakani mwa Wilaya ya Lindi na Kilwa, limetitia upande mmoja na kuhatarisha usalama wa wananchi wanaolitumia.

 Akizungumza leo Aprili 4, 2024 alipotembelea eneo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga amewaagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Taroads) wilayani humo kuhakikisha wanafanya ukarabati haraka, ili liendelee kupitika.

“Boksi la kalavati namba moja limekatika  upande mmoja, tulipata taarifa juzi na waataalamu wa Tanroads walifika, maji ni mengi, mto umeacha njia yake ya asili na kupita karibu ya barabara, tumefika kushauriana tuone tunafanya nini na tumepeana muda hadi kufika jioni tukutane tuone hiyo mipango wanayoifikiria inaweza kuzaa matunda gani,” amesema mkuu huyo wa wilaya.

Barabara hiyo ambayo ni muhimu kwa wakazi wa mikoa ya kusini mwa Tanzania, inaunganisha pia nchi jirani ikiwamo ya Msumbiji.

“Ikijifunga hatutaweza kupata bidhaa na hakutakuwa na safari za Dar es Salaam, labda tukapite Songea,” ameema Ndemanga.

Amewataka madereva wanaoendesha magari yenye uzito mkubwa kusitisha safari zao kwa sasa na magari madogo yaruhusiwe kupita moja moja upande mmoja.

"Niwaombe Tanroads mnachoona kinawezekana kufanyika sasa kifanyike haraka, ili magari yasisimame moja kwa moja,” amesema mkuu huyo wa wilaya.

Akizungumzia adha hiyo, mkazi wa Mbwemkuru,  Mohamedi Ndembo amesema;" Machi 31, saa 2 usiku nilikuwa napita na safari zangu nikakuta pamemegeka upande mmoja, nikakata majani kisha nikanza kuyaongoza magari yapite upande mmoja na siku ya pili uongozi ulifika kutazama na jana saa nane usiku daraja likaanza kutitia, lakini tuliendelea kuyaongoza magari yapite upande mmoja, ili yasikae foleni.”

Akizungumzia hilo, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Lindi, Mili  Zengo amesema sehemu ya Mto Mbwemkuru maji yamehama njia na kuja kando ya barabara na kusababisha upande wa barabara kuchimbika eneo la takriban  mita 100.

“Barabara imechimbika licha ya kuwa mvua hainyeshi maeneo haya, lakini maji yanakuja kwa wingi kutoka maeneo mengine na kusababisha kitu kama mafuriko, kwa sababu yanapita juu ya daraja,” amesema.

Amesema kwa sasa wamechukua hatua ya haraka ya kuanza kujaza mawe kwa ajili ya kulinda tuta la daraja, huku akiahidi kuchukua hatua zote ili barabara isijifunge.