Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dakika saba za Kamala Harris Makumbusho ya Taifa

Muktasari:

  • Kamala awakumbuka waliopoteza maisha kufuatia mlipuko uliotokea kwenye ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka 1998.

Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Haris ametembelea Makumbusho ya Taifa leo Alhamisi Machi 30, 2023 na kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya mabomu yaliyolipuka kwenye balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998.

Kamala ametembelea mnara huo wa kumbukumbu ambao upo katika Makumbusho ya Taifa ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu nchini Tanzania.

Kabla ya kuwasili kwake, ulinzi uliimarishwa kwenye eneo hilo kukiwa na watu wachache walioshuhudia tukio hilo wakiwemo maofisa wa ubalozi wa Marekani.

Saa 9: 34 alasiri Kamala aliwasili katika viwanja vya Makumbusho na kupokelewa na waliokuwa na wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani wakati mlipuko unatokea wakiongozwa na aliyekuwa balozi Charles Stith.

Baada ya kusalimiana na wafanyakazi hao wa zamani wa ubalozi moja kwa moja Kamala alielekea eneo ulipo mnara na kuweka shada la maua kisha kuwaombea kwa dakika moja kabla ya kuondoka.

Kamala ambaye aliwasili nchini jana saa 5:05 usiku, leo alianza kwa mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam.