Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Costech: Sekta binafsi ni chanzo cha kuendeleza ubunifu nchini

Muktasari:

  • Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (Costech) imesema sekta binafsi imekuwa chanzo na kichocheo katika kuinua  ubunifu wa vijana kwa kutoa mawazo mazuri ya kuboresha sera na kuisaidia Serikali kutoa fedha kwa kuelekeza maeneo yenye uhitaji zaidi.

Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imesema sekta binafsi imekuwa na mchango mkubwa katika kuinua ubunifu nchini kwa kutoa mawazo mazuri ya kuboresha sera.

Kauli hiyo imetolewa leo JUmatatu, Oktoba 9, 2023 na Mkurugenzi Menejimenti Maarifa, kutoka taasisi hiyo,Samson Mwela alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuelekea kwenye maonyesho ya wiki moja ya Sahara Sparks yatakayotoa fursa kwa vijana  wabunifu kuonyesha ubunifu wao.

Akizungumza katika tukio hilo, Mwela amesema Serikali imekuwa ikitenga fedha na kuingiza kwenye sekta ya kuendeleza ubunifu na ili ziweze kuelekezwa maeneo yenye manufaa na tija wanahitaji zaidi maoni ya wananchi na sekta binafsi.

“Sekta binafsi zimekuwa zikiandaa maonyesho ndani yake wanafanya mijadala inayoibua mawazo mazuri yanayokusanywa na Serikali kabla ya kuyachakata na yamekuwa msaada kufanikisha  utungaji sera na kuchochea mageuzi ya tasnia ya ubunifu nchini,”amesema

Katika maelezo yake amesema mawazo hayo mazuri yamekuwa yakiingizwa kwenye programu zao huku akieleza taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele kuweka msukumo kwenye maonyesho mbalimbali ya ubunifu wakiamini ni sehemu yenye tija kupata mawazo mapya.

Mwela amesema kupitia programu zilizoanzishwa kuanzia mwaka jana, jumla ya vijana 83 wamenufaika na mfuko wa kuendeleza ubunifu wa vijana na kati yao vijana 150 wanaotarajia kwenda kushiriki maonyesho ya Sahara wamepitia kwenye tume hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Sahara Venture, Mussa Kamata amesema tangu kuanzishwa kwa maonyesho hayo mwaka 2016 wanajivunia mafanikio mengi ikiwemo vijana 2000 wametumia fursa hiyo kuonesha ubunifu wao.

“Na Kati yao  kunawalionufaika kupata msaada wa kifedha, kutoka kwa wawekezaji ni zaidi ya vijana 12 kupitia jukwaa hili wamewezeshwa kuendeleza bunifu zao ndani na nje ya nchi,”amesema


Amesema shabaha kubwa ya kuanzisha jukwaa hilo ilikuwa ni kuwasaidia vijana wabunifu nchini kwa kuwa Tanzania hakukuwa na jukwaa kama hilo linalozungumzia masuala ya ubunifu na teknolojia tofauti na mataifa jirani yaliyokuwa yanatumia fursa hiyo.

Awali, Meneja wa taasisi hiyo, Rozi Rassa amesema maonesho hayo wanayafanya kila mwaka kwa ajili ya kunyanyua jukwaa la sayansi na teknolojia nchini kupitia ubunifu na uwekezaji.

“Tukio hili litafanyika kwa wiki nzima katika viwanda vya makumbusho ya Taifa Posta na wabunifu mbalimbali watakuwa wanaonesha bunifu zao na kutakuwa na wawekezaji watakao hudhuria kuona namna ya kuwaunga mkono,”amesema