Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

500 kushiriki kongamano la ubunifu Dar

Muktasari:

  • Kongamano hilo linaloratibiwa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (Costech) linalenga kuwakutanisha wabunifu, wataalamu ili kubailisha uzoedu na kutambua wabunifu wapya.

Dar es Salaam. Zaidi ya washiriki 500 wanatarajiwa kushiriki kongamano la nane la Sayansi na ubunifu (Stice 2023) litakalofanyika jijini hapa Juni 16- 18, likilenga kuwakutanisha wadau kubadilishana uzoefu na kukuza sayansi na teknolojia.

Akizungumza na wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari leo Juni 5 jijini hapa, Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (Costech), Dk Amos Nungu amesema kongamano hilo ni utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo ya kuishauri Serikali kuhusu maendeleo yabsayansi nabteknolojia.

"Mambo manne yatakayojadiliwa, kwanza ni fursa kwa Serikali kuhabarisha watafiti, wabunifu na wananchi mipango yake kuhusu sayansi na ubunifu.
"Pia ni fursa kwa watunga sera kupata taarifa ili ziwasaidie kufanya uamuzi. Vilevile watafiti na ubunifu wanakutana na kubadilisha uzoefu," amesema.

Amewataja washiriki watakaokuwepo kuwa ni pamoja na watatakaotoa mawasilisho, wanaokuja kuonyesha ubunifu, wataalamu wa kuendesha mijadala na wanafunzi wa shule za msingi na Sekobdari.
"Mada kuu itakuwa ni kuangalia mfumo wa wa sayansi na ubunifu na mchango wake kwa jamii.
"Katika hilo tutaangalia utayari wa serikali katika uanzishwaji wa viwanda. Pia tutaangalia uchumi wa kijani na mabadiliko ya tabianchi na mjadala wa ubunifu na maendeleo ya watu," amesema.
Pia alitaja suala la ubunifu na maemdeleo ya watu na maarifa asilia.

"Kutakuwa na maonyesho ya pembeni yakiwamo ya bayoteknolojia yakiongozwa na Ifakara Health Institute na mapnyesho ya mabadiliko ya tabia nchi na mabadiliko ya nne ya viwanda.

Katika kongamano hilo pia amesema kutakuwa na uzinduzi wa kitabu kinachoelezea matokeo ya utafiti kwa taasisi 10 zilizofadhiliwa na Costech."

Katika hatua nyingine, akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Sylvia Lupembe alisema licha ya Serikali kuwa na mwongozo wa kuwatambua wabunifu, bado inaendelea kupokea maoni ya wadau kuhusu Sera ya Elimu ili uboresha utambuzi wa wabunifu.

"Upo mwonozo wa kutambua ubunifu wa mwaka 2018. Hata hivyo, tuko kwenye mageuzi ya sera kuelekea kwenye ujuzi.
"Moja ya mambo yaliyojadiliwa ni kutambua wabunifu ambao hawakwenda shule," amesema.
Amesema kwa sasa wanaishirikisha Costech na Mamlaka ya Vyuo vya Ufundi (Veta) ili kulea bunifu.
Kwa upande wake Msimamizi wa Machapisho na Nyaraka wa Costech, Dk Bunini Manyilizu amesema kuna changamoto za wabunifu kukosa wa masoko na sayansi jamii akitaka kuwe na ushirikiano.
"Anaweza kubuni kitu, lakini hajui wananchi wanataka nini. Kwenye malaria wanasayndi wamebuni dawa, lakini lazima kuwepo kwa watafiti, watunga sera na watu wa masoko," amesema.