Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chadema yawataka Watanzania kujipanga chaguzi zijazo

Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Catherine Ruge (wapili kulia) akicheza na wanachama na wapenzi wa Chadema muda mfupi baada ya kuwasili katika viwanja vya Stendi ya Zamani mjini Mugumu kwaajili ya kuhutubia mkutano wa hadhara.  Picha na Beldina Nyakeke

Muktasari:

Chama cha Demokrasia na Manedeleo (Chadema) Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kimewaomba wakazi wa wilaya hiyo kujipanga na kukiweka madarakani katika chaguzi zijazo kwani ndicho chama pekee kinachojali maslahi ya watu bila ubaguzi.

Serengeti. Chama cha Demokrasia na Manedeleo (Chadema) Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kimewaomba Watanzania kujipanga na kukiweka madarakani katika chaguzi zijazo kikidai ndicho chama pekee kinachojali maslahi ya watu bila ubaguzi.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Jumamosi Julai 8, 2023 mjini Mugumu baadhi ya makada wa chama hicho wamesema maandalizi ya kuweka chama hicho madarakani yanatakiwa kuanza sasa.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Serengeti, Samuel Nyabahere amesema mabadiliko yanapaswa kutokea kuanzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini mwakani

“Bila kujali itikadi ya vyama tujipange tutengeneze kitu kimoja kwasababu sote tunaumia kwa yote yanayoendelea ikiwepo uongozi wa kisultani jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu," amesema

Nyabahere amesema Watanzania wanatakiwa kuchagua viongozi wanaoweza kuwaletea maendeleo endelevu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Amesema huduma za kijamii zinazotolewa haziendani na rasilimali ziliopo huku akitolea mfano upatikanaji wa huduma za afya ambazo zimekuwa ni gharama kubwa hali ambayo inapelekea watu wengi kushindwa kumudu kutokana na kuwa na uchumi mbaya.

Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Serengeti, Joseph Mwita amesema wakazi wa Wilaya ya Serengeti wanapaswa kujifunza kulingana na mambo wanayopitia kwasas baada ya halmashauri hiyo kurudi chini ya CCM mwaka 2020.

"Yapo mambo mengi yanafanyika ambayo yanatuumiza sisi hasa wananchi wenye kipato kidogo mfano kipindi chetu tulikuwa tunatoa Sh5.8 milioni kila mwezi kwaajili ya usafi lakini sasa hivi nyie ndio mnaotozwa hela kwaajili ya usafi,"amesema

Amesema inasikitisha kuona mfanyabishara anayelipa leseni ya biashara na ushuru wa huduma, tozo zingine na bado anaongezewa mzigo wa kulipia uchafu ilhali halmashauri ina uwezo huo.

"Wakati halmashauri ikiwa chini yetu tuliweza kusimamia mapati mfano mnada wa Mugumu pekee tulikuwa tunakusanya zaidi ya Sh14 milioni na ng'ombe tulikuwa tunatoza ushuru wa Sh5,000 lakini kwasasa wanatoza ng'ombe Sh7,500 sasa waulizeni mapato yako wapi na yanafanya nini,"amesema

Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Catherine Ruge amesema endapo chama hicho kitapata ridhaa ya wananchi, watanzania wataweza kunufaika na rasilimali zilizopo

"Bahati nzuri sisi Chadema tukipata  nchi tutakuwa na mfumo wa utawala wa majimbo kwahiyo kila watu wataweza kunufaika na rasilimali za maenoe yao tofauti na huu ubabaishaji wa sasa,"amesema

Amesema yapo mambo mengi yanayotokea ikiwepo masuala ya ukiukwaji wa haki za wananchi na kwamba mwenye uwezo wa kukomesha mambo hayo ni Chadema pekee.

"Watu wanauawa mfano wakazi wa vijiji vya pembezoni mwa hifadhi lakini hawana mtu wa kuwatetea nawaambia ningekuwa mbunge wa Serengeti bungeni pangechimbika sitaki utani kwenye mambo ya muhimu,"amesema

Amesema kuwa chama chake kinapigania upatikanaji wa katiba mpya ambayo itakuwa na majibu ya changamoto zote zinazowakabili wananchi.

"Tunataka wananchi wamiliki ardhi na sio kama ilivyo sasa ambapo ardhi inamilikiwa na Rais ambaye akiamua kuuza hata hifadhi yetu ya Serengeti anauza ndani ya sekunde moja,"amesema