Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bwawa la JNHPP laanza kujazwa maji

Muktasari:

Tukio la kufungwa kwa mageti ya handaki lililojengwa mwaka 2019 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) limekamilika na maji yameanza rasmi kujaa katika bwawa hilo linalotarajiwa kuzalisha megawati 2,115.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefunga rasmi geti la handaki ambalo lilijengwa kwa ajili ya kuchepusha maji ili kupisha ujenzi wa tuta la bwawa la Julius Nyerere (JNHPP).

Rais Samia amefunga geti hilo leo Desemba 22, 2022 kabla ya kutoa hotuba yake katika hafla ya kuanza kujaza maji kwenye bwawa hilo lililopo Rufiji, Mkoani Pwani.

Awali Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema ili tuta lijengwe ni lazima sehemu hiyo iwe kavu pasiwe na mto unapita hivyo walijenga handaki la kuchepusha mto ili kufanikisha ujenzi huo.

“Handaki lilikamilika mwaka 2019, mto Rufiji ukawa unapita kwenye hilo handaki na ujenzi wa tuta ukaanza na leo tumefika hatua ya kukamilika kwa tuta hili kwa kiwango cha kuweza kujaza maji na kwa kuwa kuna mvua tukaona ni wakati muafaka kwa maisha ya mradi tuzibe lile handaki ili mto huu urudi kwenye njia yake,” amesema Makamba.

Amesema maji kwa kiwango kilichotathminiwa kimazingira yataendelea kupita na kuwanufaisha wakazi wa maeneo jirani hivyo wananchi waondoe taharuki.

“Tunaziba handaki ambalo litawezesha mto Rufiji urudi kwenye njia yake ya asili handaki hili lenye mita 19 tumetengeneza geti tutakaloziba leo lenye uzito wa tani 368 na baada ya kufungwa kwa geti hili itachukua muda wa kama dakika 30 maji yataanza kujaa hapa,” amesema Waziri Makamba.