Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bodi ya Magavana yamaliza muda wake

Katibu Mkuu Wizara ya Malisasili na Utalii, Dk.Hassan Abbas akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa chuo cha Usimamizi wa wanyamapori Mweka, Profesa Faustine Bee ambaye anamaliza muda wake wa miaka 6 katika chuo hicho. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Wakati Bodi ya Magavana wa chuo cha Usimamizi wa wanyamapori, Mweka ikimaliza muda wake wa miaka 6 Serikali imesema itaendelea kuwatumia katika kuutangaza utalii na uhifadhi nchini.

Moshi. Wakati Bodi ya Magavana wa chuo cha Usimamizi wa wanyamapori, Mweka ikimaliza muda wake wa miaka 6, Katibu Mkuu Wizara ya Malisasili na utalii, Dk Hassan Abbas amesema serikali itaendelea kuwatumia katika kuutangaza utalii na uhifadhi hapa nchini.

Hayo yamebainishwa leo Jumapili Mei 28, 2023 na Katibu Mkuu Wizara ya Malisasili na utalii, Dk Hassan Abbas wakati wa shughuli ya kuiaga bodi hiyo ya Magavana wa chuo cha Usimamizi wa wanyamapori, Mweka inayomaliza muda wake.

Amesema bodi hiyo imefanya kazi kubwa na yenye kuacha alama ya vizazi na vizazi hivyo akawataka kuendelea kuwa mabalozi wa utalii hapa nchini.

"Bodi hii ambayo mnamaliza muda wenu, sio kwamba mnaondoka, bado tutawahitaji kwenye kutusaidia kwenye uhifadhi na kutangaza utalii, Rais wetu ametimiza wajibu wake kwenye kutusaidia katika eneo hilo kupitia 'Royal tour' ambapo zaidi ya Sh7 bilioni tumeiwekeza kwenye kuutangaza utalii,"

"Magavana kazi zenu zimeleta matunda mazuri na wapongeza kwa kazi kubwa mliyoifanya na imeleta matunda mengi lakini kupitia tafiti zenu mlizozifanya, mafunzo pamoja na wataalam mliowazalisha ndani ya chuo hiki," amesema

Dk Abbas alisema ubunifu, weledi na maarifa ndio misingi mikubwa ambayo itasaidia kupeleka mbele gurudumu la utalii hapa nchini hasa katika chuo hicho ambacho msingi wake mkubwa ni kutoa taaluma ya uhifadhi pamoja na mambo mengine.

Akizungumzia bodi hiyo, Mkuu wa chuo cha Mweka, Profesa Jafary Kideghesho amesema uwepo wa bodi hiyo ya Magavana katika chuo hicho imeleta mabadiliko chanya na kukiwezesha chuo hicho kutekeleza kwa ufanisi majukumu yake ya msingi ya kutia mafunzo, kufanya tafiti pamoja na ushauri wa kitaalam na ugani.

"Bodi hii wakati inateuliwa mara ya kwanza hali ya chuo haikuwa kama ilivyo sasa, eneo la taaluma limeimarika kutokana na kupitiwa upya mitaala na kuanzisha upya programu zinazojibu mahitaji ya soko katika eneo la uhifadhi pamoja na maeneo mengine,"

"Alama iliyoachwa na bodi hii  itashuhudiwa na vizazi vijavyo,  kazi iliyofanyika kwa miaka sita imeweka mwanzo mzuri wa bodi mpya itakayoteuliwa, hata hivyo chuo kama mdau mkubwa wa uhifadhi na utalii tunapongeza hatua zinazochukuliwa na serikali kuokoa uhifadhi, mifumo mbalimbali ya ikolojia na wanayanapori nchini pamoja na jitihada mbalimbali zinazoendela za kukuza utalii nchini," amesema Profesa Kideghesho.

Naye, Mwenyekiti wa bodi ya Magavana anayemaliza muda wake, Profesa Faustine Bee amesema baada ya bodi hiyo kuteuliwa mwaka 2016 yamekuwepo mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongeza kiwango cha ubora wa taaluma kwa wanataaluma na wasio wanataaluma kuhakikisha wanapata mafunzo ya kujengewa uwezo unaohitajika.

"Kwa kipindi chote cha miaka 6 ambayo inaishia Juni 13, mwaka tumeweza kuongeza kiwango cha ubora wa taaluma inayotolewa hapa chuoni, ikiwa ni kuboresha mitaala kuendana na uhitaji wa sasa wa soko,"