Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Biteko kuzindua mnara wa kumbukumbu Mweka

Muktasari:

  • Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko kesho, Novemba 25, 2023 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya miaka 60 na mahafali ya 59 ya  chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Afrika, Mweka, mkoani Kilimanjaro.

Moshi. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko kesho, Novemba 25, 2023 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya miaka 60 na mahafali ya 59 ya  chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Afrika, Mweka, mkoani Kilimanjaro.

Taarifa hiyo imetolewa leo, Novemba 24 na Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Ernest Emmanuel wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa, ambapo amesema pamoja na maadhimisho hayo atazindua mnara wa kumbukumbu ya miaka 60 ya chuo hicho pamoja na kutunuku vyeti kwa wahitimu wa chuo hicho.

Pamoja na mambo mengine atashiriki shughuli mbalimbali zitakazofanyika chuoni hapo ikiwemo upandaji wa mti wa kumbukumbu.

"Kesho Novemba 25, tutakuwa na ujio wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati katika chuo chetu cha Mweka, ambapo atashiriki kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya chuo hiki na mahafali ya 59 tangu kuanzishwe kwake mwaka 1963,"

"Shughuli atakazozifanya hapa chuoni kwetu, atazindua mnara wa kumbukumbu ya miaka 60 ya chuo hiki, kuotesha mti wa kumbukumbu, kutoa vyeti kwa wahitimu wa ngazi mbalimbali hapa chuoni,"amesema Ernest

Tangu chuo hicho kianzishwe mwaka 1963, kimefanya tafiti mbalimbali katika kutatua changamoto za masuala ya uhifadhi wa wanyamapori nchini  na kimezalisha wahitimu zaidi ya 11,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani.