Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Basi lakamatwa likiwa limebeba wanafunzi 62 usiku Iringa

Muktasari:

  •  Licha ya kutengenezwa baada ya kuharibika, Jeshi la Polisi, Kitengo cha Usalama Barabarani, Mkoani Iringa limezuia basi la Kimotco lililokuwa limebeba wanafunzi 62 na walimu saba wa Shule ya Msingi Camaldoli wilayani Mufindi lisiendelee na safari.

  




Iringa.  Licha ya kutengenezwa baada ya kuharibika, Jeshi la Polisi, Kitengo cha Usalama Barabarani, Mkoani Iringa limezuia basi la Kimotco lililokuwa limebeba wanafunzi 62 na walimu saba wa Shule ya Msingi Camaldoli wilayani Mufindi lisiendelee na safari.

Jeshi hilo lilimelazimika kulizuia basi hilo baada ya kubaini halina mikanda ya abiria jambo ambalo ni hatari watoto.

Pia, basi hilo linadaiwa kuanza safari saa saba usiku kinyume cha sheria huku likiwa halijakaguliwa wala kupewa kibali cha kusafirisha wanafunzi.

Basi hilo limezuiwa wakati ikiwa zimepita siku chache baada ya wanafunzi 11 wanaosoma shule ya King David kupoteza maisha baada ya basi lao kutumbukia shimoni katika eneo la Mjimwema, Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mkoani Mtwara.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama, Barabarani Mkoani Iringa, Mosi Ndozero amesema ni kosa kisheria kwa basi lolote linalobeba wanafunzi kuanza safari usiku wa manane na bila kibali maalum cha kusafirisha abiria hao.

“Hii iwe ni onyo kwa mabasi mengine yote, ni marufuku kupakia wanafunzi bila kibali na kukaguliwa, lakini pia sheria hairuhusu safari za usiku.

“Basi hili nalichukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho. Mmeondoka usiku wa manane vipi kama lingetokea lolote,” amesema.

Hata hivyo, baada ya basi hilo kutengenezwa kifaa kilichokuwa kimeharibika, ukaguzi wa polisi ulibaini halina mikanda kwa ajili ya abiria jambo lililomfanya Ndozero kuzuia lisiendelee na safari.

Mwalimu wa shule hiyo na mkuu wa msafara, Valence Ndembela walikiri walianza safari usiku wa manane kwa shinikizo la wenye gari.

Alisema awali, walikuwa wanawasiliana na wakala wa basi hilo, Agrey ambaye aliwahakikishia kuwa basi ni zima na limefanyiwa ukaguzi.

Kwa upande wake, wakala wa basi hilo, Agrey amesema  japo wanafunzi hao walipakiwa kwenye mabasi mengine mawili, mkoani Dodoma watarejeshwa kwenye basi jingine la kampuni yao lililokaguliwa.